Senegar yaanza kwa kutoa kichapo Afcon, leo ni Ivory Coast na Togo ya Bossou
Senegar wameanza vema michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tunisia katika kundi B.
Tunisia wangeweza kupata bao katika dakika ya pili ya mchezo, pale Ahmed Akaichi alipipata fursa nzudi na kuupiga mpira kupitia kichwa lakini akatoka nje.
Senegar ilipata bao la kwanza kupitia mkwaju wa penalti uliopigwa na winga Sadio Mane.
Tunisia walikosa nafasi nyingi za wazi hasa Youssef Msakni, ushindi wa vijana wa Allou Cisse umeifanya timu hiyo kuwa kileleni mwa msimamo wa kundi lao.
Zimbabwe nao walitoka sare ya 2-2 na Algeria kwa magoli ya Kudakwashe Mahachi na Nyasha Mushekwi na yale ya Riyad Mahrez yalitosha kukifanya pambano hilo kuwa droo, Leo Togo na Ivory Coast zimeumana vikali na hadi mwisho zilitoka suluhu 0-0