DRC yailipua Morocco, Afcon

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeweka matatizo yake pembeni na kuicharaza Morocco kwa bao 1-0 kwenye mchezo wake wa ufunguzi wa kombe la mataifa ya Afrika nchini Gabon.

Kikosi cha Froribert Ibenge kilchofanya mgomo siku ya Ijumaa kutokana na kutolipwa bakshishi zao, almanusura wafungwe bao la mapema kwenye Uwanja wa Stade d'0yere, baada ya Mbarak Boussoufa kugongesha mwamba shuti lake.

Junior Kabanaaga ndiye aliyewainua mashabiki wa DRC baada ya kufunga bao pekee katika dakika ya 55 kipindi cha pili, DRC walimaliza wakiwa mchezaji mmoja pungufu baada ya Lomalisa Mutambala kutolewa nje kwa kuonyeshwa kadi mbili za manjano.

Mutambala aliingia kama mchezaji wa akiba, na kutolewa baada ya dakika 16, Youssef El Araba wa Morocco alishindwa kufunga katika nafasi mbili alizopata kwa kichwa, mwishoni mwa mchezo.

DRC walilazimika kucheza wakiwa tisa tu uwanjani kwa muda baada ya Mutambala kutolewa na beki Gabriel Zakuani kuumia na kutoka nje, Congo Kinshasa sasa inaongoza kundinC baada ya mchezo wa awali kati ya mabingwa watetezi Ivory Coast kutoka sare 0-0 na Togo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons