BURKINA FASO, CAMEROON SARE SARE MAUA AFCON, DIAMOND ACHIZISHA WATAZAMAJI
Burkina Faso imeilazimisha sare Cameroon ya kufungana mabao 1-1 katika mechi yao ya kwanza ya AFCON mjini Libreville nchini Gabon.
Mechi hiyo ilionekana kama ya Cameroon ambao walitangulia kupata bao katika dakika ya 35 mfungaji akiwa ni Benjamin Moukandjo na likadumu hadi mapumziko.
Lakini Issoufou Dayo aliisawazishia Burkina Faso katika dakika ya 75 na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare sare maua.
Mwanamuziki wa miondoko ya kizazi kipya kutoka nchini Tanzania, Diamond Platinum alitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa michuano hiyo, Diamond aliwachizisha watazamaji na kuonekana wakimshangilia kwa kupiga makofi