Machapisho

Telela atoboa kilichompeleka Ndanda

Picha
Na Saida Salum, Mtwara Kiungo wa zamani wa Yanga SC, Salum Abdul Telela 'Abo Master' ametoboa siri yake ya kujiunga na Ndanda ya Mtwara badala ya Simba SC na Mwadui ambazo zilionyesha nia ya kutaka kumsajili. Akizungumza na mtandao huu, Telela amesema, kilichompeleka Ndanda ni masomo kwani kwa sasa anasoma katika chuo kishiriki cha Stella Maris ambapo tawi lake lipo Mtwara. Telela amedai mpira ni sehemu ya maisha yake lakini elimu ni kitu muhimu kwake, kiungo huyo ametemwa na Yanga lakini bado yupo kwenye kiwango kizuri cha kutandaza soka

Mo amwaga mamilioni Msimbazi

Picha
Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam Mfanyabiashara mkubwa nchini na mpenzi wa klabu ya Simba Mohamed Dewji 'Mo' leo ametimiza ahadi yake baada ya kuimwagia klabu hiyo Shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia usajili. Mo ambaye aliahidi kusaidia fedha za usajili endapo wanachama wa klabu hiyo wangemkubalia ombi lake la kutaka kuinunua Simba, Mwishoni wiki iliyopita klabu ya Simba ilifanya mkutano wake wa wanachama ambapo waliridhia kuuzwa kwa klabu hiyo. Naye rais wa Simba, Evans Aveva amefurahishwa na Mo kumpatia fedha hizo kwani hali yao kifedha kwa sasa si nzuri, Aveva pia amewataka Wanasimba wengine kumuiga Mo na kujitolea na kusaidia

AZAM YAMALIZANA NA MBAYA WA YANGA

Picha
Na Salum Fikiri Jr  DAR ES SALAAM KLABU bingwa Afrika mashariki na kati Azam FC imefanikiwa kumsainisha winga machachari wa Medeama ya Ghana Enock Atta Agyoi kwa mkataba wa miaka miwili. Atta alikuwa tishio kwa mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga SC katika mchezo wa makundi kombe la Shirikisho dhidi ya Medeama, katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Taifa Dar es Salaam  Yanga ililazimishwa sare ya kufungana 1-1. Ina maana Ataa ataitumikia Azam FC msimu ujao na katika mchezo wa Ngao ya Hisani ambapo Azam itakutana na Yanga katika uwanja wa Taifa

SIMBA YAIBOMOA TENA AZAM

Picha
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM BAADA ya kufanikiwa kumsana mshambuliaji hatari Ally Ame 'Zungu', Klabu ya Simba imeendelea kuibomoa Azam, Na safari hii ikifanikiwa kumnasa mlinda mlango mahiri Mwadini Ally Mwadini ambaye pia ni kipa wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes. Habari zenye uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa, Mwadini amesainishwa mkataba wa miaka miwili na atakipiga kwenye klabu hiyo hadi mwaka 2018. Mwadini hakuwa na wakati mzuri alipokuwa Azam ambapo alikuwa akiwekwa benchi la kipa bora wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/16 Aishi Manula, hata hivyo Mwadini asingeweza kurejea langoni kwani timu hiyo imemleta kipa wa kombe la Dunia raia wa Ivory Coast

SIMBA SASA YAMRUDISHA LOGARUSIC

Picha
Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM SIMBA SC sasa ni kama inamrudisha kocha wake wa zamani Mcroatia Zdravko Logarusic hasa baada ya kuipa mwaliko timu yake mpya ya Interclube ya Angola ambapo sasa itakuja kucheza na Simba katika tamasha la Simba Day katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Awali Simba iliialika Gor Mahia ya Kenya lakini sasa imeamua kuialika Interclube ya Angola moja kati ya vilabu vikubwa nchini humo, Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva amesema leo kwamba Simba itacheza na Interclube na itatambulisha kikosi chake chote. Aveva amedai mbali na kutambulisha  kikosi kipya, Simba pia itatambulisha jezi zake mpya itakazotumia kwenye Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba itafungua na Ndanda FC 'Wana-Kuchele'

MO SASA KUKABIDHIWA TIMU JULAI 30

Picha
Na Saida Salum, DAR ES SALAAM UONGOZI wa klabu ya Simba umeonyesha nia ya kumkabidhi klabu hiyo mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewji "Mo". Mambo Uwanjani imezipata taarifa za ndani kabisa ambazo zinasema kwamba Mo anakabidhiwa timu hiyo Julai 30 mwaka huu ambapo kutafanyika mkutano mkuu wa wanachama. Katika mkutano huo, wanachama wa Simba wataamua wenyewe kama klabu yao iendeshwe kisasa yaani kampuni ama iendelee na mtindo uleule wa wanachama. Endapo Simba itachagua kuwa kampuni basi ni sawa kama wamempa klabu hiyo Mo ambaye ameonyesha nia kubwa ya kuinunua timu hiyo, Mo anataka kuinunua Simba kwa shilingi Bilioni 20 ni sawa na kuinunua Simba kwa asilimia 51 na hisa nyingine atawaachia Simba wenyewe

AMOSI KIPANDE, ANAYEJIANDAA KULIZIBA PENGO LA MR EBBO

Picha
Katika Burudani Leo Taunamzungumzia Mwahiphop Amosi Mkama A.K.A Boss Rapper Ama Kipande Na Wana. Msanii Pekee Ambaye Anaweza Kuliziba Pengo La Marehemu Mr Ebbo. Kutokana Na Mashaili Yake Mazuri Yenye Ujumbe Wa Kuchekesha Na Kufundisha. Ukweli Utabaki Kuwa Ukweli Pale Alipo Achia Nyimbo Yake Iitwayo Pesa Shobo. Aliyowashirikisha  Golo Man Na Moriento Katika studio Ya Hekiman Records Chini Ya Producer Galatone Money Na Meneja Sakaingo. Nyimbo Iliyo Mpa Mashabiki Wengi Sana Na Kujipatia Shoo Mbalimbali. Kwa Sasa Yuko Jikoni Akiipika nyimbo Yake Mpya Itwayo Shori Wa Kijiji. Amboyo Ameshindwa Kuniweka Wazi Atafanya Nanani, Amapekeyake Au Studio Gani. Aliniambia Ukuacheka Kama Kawaida Yake Akisema Uhusio Muda Wakuongea Kila Kitu Ila Mashabiki Wangu Wategemee Mambo Manzuri Kutoka Kwangu. Nimimi Mkola Man Kutoka Hale Ktk Habari Na Wasanii