Telela atoboa kilichompeleka Ndanda

Na Saida Salum, Mtwara

Kiungo wa zamani wa Yanga SC, Salum Abdul Telela 'Abo Master' ametoboa siri yake ya kujiunga na Ndanda ya Mtwara badala ya Simba SC na Mwadui ambazo zilionyesha nia ya kutaka kumsajili.

Akizungumza na mtandao huu, Telela amesema, kilichompeleka Ndanda ni masomo kwani kwa sasa anasoma katika chuo kishiriki cha Stella Maris ambapo tawi lake lipo Mtwara.

Telela amedai mpira ni sehemu ya maisha yake lakini elimu ni kitu muhimu kwake, kiungo huyo ametemwa na Yanga lakini bado yupo kwenye kiwango kizuri cha kutandaza soka

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons