Machapisho

GEORGE BUSH ALAZWA MAREKANI

Picha
Aliyekuwa rais wa Marekani George H.W Bush amekimbizwa katika hospitali moja ya Houston nchini Marekani baada ya kupatikana na tatizo la kupumua. Kulingana na madaktari,Bush mwenye umri wa miaka 90 anachunguzwa katika hospitali ya Methodist. Alipelekwa katika hospitali hiyo na ambalensi jumanne usiku. Wawakilishi wa Bush wanasema kuwa hatua hiyo ya kupelekwa hospitali ni kama tahadhari.

RA,OS AMALIZA MWAKA BORA KWA TUZO YA CWC

Picha
Sergio Ramos Difenda wa Real Madrid aliyeshinda mataji mengi Sergio Ramos ametaja mwaka 2014 "mwaka bora zaidi maishani mwangu” baada ya kuchangia sana ufanisi wa miamba hao wa Uhispania waliposhinda mataji manne ikiwa ni pamoja na kutwaa kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara ya 10. Mkabaji huyo wa kati ambaye nguvu zake angani mara nyingi huzalisha mabao alishinda tuzo ya mchezaji wa dimba katika Kombe la Dunia la Klabu baada ya kufunga wakati wa ushindi nusufainali dhidi ya Cruz Azul na ushindi dhidi ya San Lorenzo kwenye fainali Jumamosi. Tukio kuu zaidi uwanjani katika mwaka ambao pia alikuwa baba kwa mara ya kwanza lilikuwa kusawazisha dakiak za mwisho dhidi ya Atletico Madrid fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya Mei kabla ya Real kushinda mahasimu hao wao wa jiji 4-1 baada ya muda wa ziada kuongezwa.

MESSI ATOSWA CHELSEA

Picha
Kocha wa Timu ya Chelsea Jose Mourinho amesema kwa sasa hawana nafasi ya kumsaini mchezaji Lionel Messi kwa kuwa hakuna Fedha ya kutosha kumsajili mchezaji huyo .

MOURINHO AFURAHISHWA SANA NA VIJANA WAKE

Picha
Jose Mourinho Meneja wa Chelsea Jose Mourinho alisifu sana ushindi wa vijana wake wa 2-0 Ligi ya Premia ugenini Stoke City Jumatatu na kuutaja kuwa mojawapo ya ushindi muhimu zaidi wao msimu huu. Bao la kichwa dakika ya pili kutoka kwa John Terry na la Cesc Fabregas kipindi cha pili, yaliwezesha vijana hao wa London kurejesha mwanya wa alama tatu kileleni mwa jedwali kati yao na Manchester City klabu zikielekea Krismasi. Lakini ni jinsi ushindi huo ulivyopatikana iliyomfurahisha Mourinho sana huku Chelsea wakipigana kushinda vita vikali vya kimwili. “Kushinda hapa lazima ucheze mchezo mzuri sana na tulifanya hivyo kwa sababu tulibadilika na mtindo wao wa uchezaji,” akasema. “Tulipokuwa na mpira, tulijaribu kutopoteza sifa zetu na kucheza mchezo wetu. “Huwa wakali sana uwanja huu, na mashabiki huwaunga mkono sana. Wana wachezaji wazuri na benchi zuri pia. Ulikuwa ushindi mgumu.

MAJANGA YANGA, MLIBERIA WAKE ASAKWA ULAYA

Picha
WAKATI Yanga ikiwa katika maandalizi ya mwisho kuwavaa Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara, jambo jipya limeibuka kuwa yule mshambuliaji wake hatari, Kpah Sherman raia wa Liberia, anatuhumiwa kutoroka kazini nchini Cyprus Kaskazini. Taarifa kutoka Cyprus Kaskazini barani Ulaya kwa mmoja wa Watanzania wanaoishi nchini humo zimeeleza vyombo vya habari nchini humo, vimeripoti kuwa Mliberia huyo atafunguliwa mashitaka baada ya kutorokea Tanzania. “Nimesikia huyo mchezaji yuko huko nyumbani, ila huku vyombo vya habari vya hapa vimeripoti timu yake ina mpango wa kufungua kesi Fifa kuelezea kuhusiana na kutoroka kwake,” alisema Mtanzania huyo anayeishi nchini humo. Juhudi za kuwapata viongozi wa Yanga ilikuwa ni ‘sheedaa’, imeelezwa Mwenyekiti Yusuf Manji yuko nje ya nchi na katibu mkuu mpya, hajaingia ofisini rasmi. Uongozi wa Klabu ya Centikaya TSK ya Cyprus, umethibitisha kushitushwa na taarifa za Sherman kuondoka nchini humo akidai ana matatizo ya kifamilia.

MAKALA: YAJUE MAISHA YA JONAS MKUDE WA SIMBA SC

Picha
TANZANIA ina jumla ya watu milioni 45 kulingana na sensa ya watu ya mwaka 2012, kati yao kuna wanandinga lukuki, lakini ina kiungo mmoja tu mkabaji anayeaminiwa na wengi ambaye si mwingine ni Jonas Gerald Mkude utotoni alikuwa akiitwa Jonas Mwakindagi. Wengi hawaijui historia ya Mkude lakini gazeti la Msimbazi limefanikisha kuipata na hatimaye leo inawajuza, alipokuwa mdogo akicheza mpira wa chandimu, Mkude alianzia golini. Timu ya mtaani kwake iliyoanzia kucheza barabarani na kupelekea usumbufu mkubwa kwa wapita njia, hasa watembea kwa miguu, baiskeli au magari na pikipiki, Mkude na akiwa na umri wa miaka minne alisimama imara katika lango la timu yake. Kipindi hicho alipata usumbufu mkubwa kutoka kwa mama yake ambaye hakutaka mwanaye acheze soka, lakini alijiiba mara kwa mara na kuendelea nao.

PHIRI ASEMASIMBA SASA IMEIVA, ANAYEKATIZA MBELE HALALI YAO

Picha
Baada ya kuichapa Yanga mabao 2-0 na kufanikiwa kunasa saini za nyota watatu wapya kutoka Uganda, kocha wa Simba, Mzambia Patrick Phiri alisema kikosi chake sasa kimeiva na anaamini kitafanya kazi nzuri msimu huu. Simba iliinyanyasa bila huruma Yanga kwa kuipa kipigo cha pili katika mechi ya Nani Mtani Jembe 2 iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi. Katika mechi hiyo, Simba iliwatumia wachezaji wawili kutoka Uganda waliokuwa wametua nchini kwa ajili ya kufanya majaribio, beki Juuko Murshid na mshambuliaji Simon Sserunkuma kabla ya juzi kuwasanisha mikataba baada ya kuridhika na viwango vyao. Katika mahojiano na NIPASHE jijini jana, Phiri alisema kikosi chake kimeimarika na kinampa matumaini ya kufanya vizuri katika mechi zinazofuata za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu baada ya kuanza vibaya katika mechi sita za awali walizoambulia sare. "Kesho (leo) tutaanika wachezaji wote walioingia na kutoka Simba kabla ya timu yetu kuingia kambini Ndege...