MOURINHO AFURAHISHWA SANA NA VIJANA WAKE

Jose Mourinho

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho alisifu sana ushindi wa vijana wake wa 2-0 Ligi ya Premia ugenini Stoke City Jumatatu na kuutaja kuwa mojawapo ya ushindi muhimu zaidi wao msimu huu.

Bao la kichwa dakika ya pili kutoka kwa John Terry na la Cesc Fabregas kipindi cha pili, yaliwezesha vijana hao wa London kurejesha mwanya wa alama tatu kileleni mwa jedwali kati yao na Manchester City klabu zikielekea Krismasi.

Lakini ni jinsi ushindi huo ulivyopatikana iliyomfurahisha Mourinho sana huku Chelsea wakipigana kushinda vita vikali vya kimwili.
“Kushinda hapa lazima ucheze mchezo mzuri sana na tulifanya hivyo kwa sababu tulibadilika na mtindo wao wa uchezaji,” akasema.

“Tulipokuwa na mpira, tulijaribu kutopoteza sifa zetu na kucheza mchezo wetu.
“Huwa wakali sana uwanja huu, na mashabiki huwaunga mkono sana. Wana wachezaji wazuri na benchi zuri pia. Ulikuwa ushindi mgumu.


“Ni ushindi ambao una maana zaidi ya alama tatu. Haikuwa tu vigumu lakini unahitaji zaidi ya ustadi wako pekee kushinda hapa.

“Wachezaji walikabiliana vyema na mtindo huo mgumu na hawakuogopa kuwajibika na wachezaji wetu wabunifu hawakuogopa kukabili mechi.

"Wachezaji wetu wa kujilinda walikuwa ngangari sana. Ni kwa kuwa na uchezaji mzuri sana wa timu ambapo iliwezekana kushinda Stoke.”

Mourinho pia alimsifu nahodha wake Terry aliyefunga katika Ligi ya Premia kwa msimu wa 15 mfululizo.
“Huwa hatari sana michezo ya kupangwa, ni mchezaji mzuri sana angani, daima huwa hatari,” akasema.
“Muhimu zaidi ni jinsi amekuwa akicheza msimu huu tena. Nilipofika hapa mwaka jana alikuwa katika matatizo kiasi, uchezaji wake ulikuwa na panda shuka. Hakuwa akichezea Chelsea sana.
"Lakini ghafla miaka miwili iliyopita, anacheza karibu kila mechi na kwangu katika kiwango sawa ana alichokuwa nilipokuwa hapa 2004-2007.

"Ni kutokana na njia yetu ya kufanya kazi. Aliingiliana vyema sana na njia yetu ya mazoezi na mwili wake.
"Anajihisi mkali na mwenye kasi katika hali nzuri, Ana furaha na unapokuwa na furaha na unajiamini basi huwa rahisi katika kila kazi. Kandanda huhitaji sana hili. Anajua namwamini na ana imani na anacheza vyema sana.”

Mkabaji kamili wa Stoke Phil Bardsley alionyeshwa kadi ya njano pekee kwa kumpiga ngwara nyota wa Ubelgiji Eden Hazard kipindi cha kwanza lakini Mourinho, aliyechemka sana wakati huo, alifikiri alifaa kufukuzwa uwanjani.

“Kwa maoni yangu na mwilini, inaonekana kama ilikuwa kadi nyekundu lakini sijui,” akasema Mourinho.
"Nijuacho ni kwamba ikiwa alicheza visivyo, kilikuwa kisa pekee. Ilikuwa mechi safi lakini ya kukaripiana sana. Refa alidhibiti mechi. Wachezaji walicheza haki.

“Vilikuwa vita vyema. Nguvu za mwili, kukabiliana moja kwa moja, mipira mingi ya mbali. Lakini mechi ilikuwa safi kabisa na sahihi. Iwapo ilikuwa kadi nyekundu kilikuwa kisa pekee. Na tunahitaji kutilia maanani hilo.”

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA