RA,OS AMALIZA MWAKA BORA KWA TUZO YA CWC

Sergio Ramos

Difenda wa Real Madrid aliyeshinda mataji mengi Sergio Ramos ametaja mwaka 2014 "mwaka bora zaidi maishani mwangu” baada ya kuchangia sana ufanisi wa miamba hao wa Uhispania waliposhinda mataji manne ikiwa ni pamoja na kutwaa kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara ya 10.

Mkabaji huyo wa kati ambaye nguvu zake angani mara nyingi huzalisha mabao alishinda tuzo ya mchezaji wa dimba katika Kombe la Dunia la Klabu baada ya kufunga wakati wa ushindi nusufainali dhidi ya Cruz Azul na ushindi dhidi ya San Lorenzo kwenye fainali Jumamosi.
Tukio kuu zaidi uwanjani katika mwaka ambao pia alikuwa baba kwa mara ya kwanza lilikuwa kusawazisha dakiak za mwisho dhidi ya Atletico Madrid fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya Mei kabla ya Real kushinda mahasimu hao wao wa jiji 4-1 baada ya muda wa ziada kuongezwa.


Mabao yake dhidi ya Cruz Azul, San Lorenzo na Atletico yalikuwa ya kawaida ya ufungaji kwa kichwa michezo ya kupangwa na ilitia nguvu zaidi nafasi ya mzaliwa huyo wa Seville mwenye miaka 28 kama shujaa miongoni mwa mashabiki wa Real.

Ramos mwenye chale nyingi pia alikuwa mchezaji muhimu kwenye timu ya Uhispania iliyoshinda mfululizo mataji ya Ubingwa Ulaya 2008 na 2012 na Kombe la Dunia mara ya kwanza hapo katikati.
Kushindwa kwa Uhispania kutetea taji la Kombe la Dunia Brazil mwezi Juni kuliwa doa kuu lakini Ramos hata hivyo alitangaza mwaka 2014 kama “muhimu zaidi maishani mwangu, uwanjani na maisha yangu binafsi.”

"Nilikuwa na tukio kuu la kuwa baba na kwenye uchezaji niliweza kushinda mataji manne na kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ambalo tulitaka sana,” aliambia kituo cha redio cha Cadena Ser baadaye Jumapili.
“Kushinda tuzo hufurahisha sana lakini ni kupitia bidii ya wachezaji wenzangu na ikiwa mchezaji binafsi anang’aa ni kutokana na juhudi zao.”

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA