Machapisho

LOGA AKALIA KUTI KAVU SIMBA,WACHEZAJI WAMCHONGEA KWA RAGE

Picha
WACHEZAJI wa Simba SC wameahidi kwenda kupigana kufa na kupona kwa ajili ya ushindi dhidi ya Mbeya City Jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Kikao cha juzi baina ya wachezaji wa klabu hiyo na Mwenyekiti wao, Alhaj Ismail Aden Rage makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi kilimalizika vizuri, japokuwa kilianza vibaya. Baada ya Mwenyekiti kuhoji juu ya kufungwa na Mgambo JKT 1-0 Jumapili Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wachezaji walitoa sababu lukuki.

DAVID LUHENDE: KUTOKA BEKI HADI USHAMBULIAJI.

Picha
Na Prince Hoza DAVID Luhende kwa sasa anasifika kama kiungo mshambuliaji na amekuwa tishio katika kikosi cha Yanga, kuwepo kwake kumeongeza chachu katika safu ya ushambuliaji na kuifanya timu yake kung'ara. Mwishoni mwa juma lililopita, Yanga iliibuka na ushindi mnono wa mabao7-0 dhidi ya Komorozine De Dimono ya jamhuri ya watu wa Comoro, ushindi huo mkubwa kwa klabu ya Yanga pengine ni wa kwanza katika uwanja wa Taifa. Yanga inakuwa timu ya kwanza kuibuka na ushindi mkubwa, timu nyingine iliyopata ushindi mkubwa katika uwanja huo ni Simba SC anbayo iliifunga Mgambo JKT ya Tanga mabao 6-0. Lakini ushindi wa Simba ulikuwa wa ligi kuu Tanzania bara tofauti na Yanga ambao ushindi wao ni wa michuano mikubwa kuliko yote kwa upande wa vilabu Afrika, yaani ligi ya mabingwa barani Afrika. Yanga imepata ushindi huo katika mkondo wa kwanza na inatarajia kurudiana nayo mwishoni mwa wiki hii mchezo utakaopigwa huko Moroni mji mkuu wa Comoro. Endapo Yanga itapata sare ya aina yoyote ile au kufu...

TRA YAUA UCHUMI WA KARIAKOO.

Picha
Na Regina Mkonde Hii yapata mara mbili zaidi kwa wafanyabiashar wa Kariakoo kuweka mgomo.Toka jana wafanya biashara hao wa kariakoo wamegoma kufungua maduka yao kutokana na ongezeko la ushuru,gharama zinazotarajiwa kuongezwa na TRA(TANZANIA REVENUE AUTHORITY.) Mgomo huu umehusishwa zaidi na wafanya biashara walipao kodi. Chanzo kilichopelekea mgomo huu kuanza tena jana ,ni baada ya TRA kuzidi kukazia msimamo juu ya matumizi ya mashine hizo.ambapo wahusika wanaohitajika kutumia mashine hizo ni wale wafanyabiashara wenye mitaji kuanzia Mil 4 Tsh na kuendelea. Wafanya biashara wamelalamika juu ya mfumo huo kutokana na gharama zinazotokana na mfumo huo,kwanza hizo mashine zinazofahamika kwa jina la ELECTRONIC FISCAL DEVICE(EFD)   na inafahamika kwamba huuzwa kwa sh laki nane,hivyo si wote qambao wenye pesa kwa sasa kwa ajili ya kuknunua mashine hiyo,na kuzidi kuacha wafanya biashara kwenye mgomo mpaka sasa.

AZAM YAANZA VYEMA KIMATAIFA.

Picha
AZAM FC jana ilianza vyema kampeni zake za kuwania ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuifunga klabu ya Ferroviario de Beira ya Msumbiji kwa goli 1-0 katika mechi yao ya kwanza ya hatua ya kwanza ya raundi ya awali kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam. Kipre Tchetche alifunga goli la kwanza kwa Azam baada ya kupata pasi ya Brian Umony na kupiga shuti kali lililomshinda kipa wa Ferroviario, Willard Manyatera na kutinga wavuni katika dakika ya 41. Wenyeji Azam walianza vyema mechi hiyo kwa kulishambulia lango la Ferroviario tangu mapema. Khamis Mcha alikuwa katika nafasi ya kufunga katika dakika ya nne tu ya mchezo lakini shuti lake liliokolewa na beki Reinildo Mandava.

MGAMBO JKT YAICHAKAZA SIMBA MKWAKWANI.

Picha
Simba ilipoteza nafasi ya kusogea zaidi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara wakati ilipokubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa timu iliyokuwa ikishika mkia ya Mgambo kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga jana. Kilikuwa ni kisasi kizuri kwa Mgambo ambayo katika mechi yao ya mzunguko wa kwanza msimu huu ilisambaratishwa kwa magoli 6-0 dhidi ya Wekundu hao wa Msimbazi huku mshambuliaji Amisi Tambwe akiweka rekodi mpya ya 'hat-trick' iliyomshuhudia akifunga magoli manne jioni hiyo. Matokeo hayo yanaifanya Simba kuanguka kwa nafasi moja hadi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 31, tatu nyuma ya Mbeya City iliyopanda hadi nafasi ya tatu kwenye ligi baada ya jana kuifunga Mtibwa Sugar 2-1 kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

DARREN BENT AINYIMA USHINDI MAN UNITED

Picha
BAO la dakika ya mwisho la Darren Bent limeinyima ushindi Manchester United baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 nyumbani Uwanja wa Old Trafford na Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. Baada ya Fulham kupata bao la kuongoza kupitia kwa Steve Sidwell dakika ya 19, United ilipata mabao mawili ya haraka haraka na kuongoza mchezo kupitia kwa Robin van Persie dakika ya 79 na Michael Carrick 80.

MKOLA MAN, YUSA G USO KWA USO NA NEY WA MITEGO, DIAMOND

Picha
Na Exipedito Mataruma STAA wa Hip Hop kutoka pande za Hale mkoani Tanga Christopher Mhenga 'Mkola Man' pamoja na mshirika wake Yusa G wameingia mafichoni kwa ajili ya kuwakabili na kuwashinda magwiji wawili waliovuma katika wimbo wa 'Muziki gani' Naseeb Abdul 'Diamond Plutinum' na Emmanuel Elibarik maarufu Ney wa Mitego katikasiku ya wapendanao Valentine Day. (Pichani Mkola Man aliye kushoto akiwa na mshirika wake Yusa G) Wawili hao wenye majina makubwa hapa nchini huenda wakatua jijini Tanga kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wao katika kilele cha siku ya wapendanao itakayoadhimishwa Februali 14, Mkola Man na Yusa G wanaamini shoo hiyo itafanyika jijini Tanga lakini wamesema watawasubiri kwa hamu kubwa.