TRA YAUA UCHUMI WA KARIAKOO.
Na Regina MkondeHii yapata mara mbili zaidi kwa wafanyabiashar wa Kariakoo kuweka mgomo.Toka jana wafanya biashara hao wa kariakoo wamegoma kufungua maduka yao kutokana na ongezeko la ushuru,gharama zinazotarajiwa kuongezwa na TRA(TANZANIA REVENUE AUTHORITY.) Mgomo huu umehusishwa zaidi na wafanya biashara walipao kodi.
Chanzo kilichopelekea mgomo huu kuanza tena jana ,ni baada ya TRA kuzidi kukazia msimamo juu ya matumizi ya mashine hizo.ambapo wahusika wanaohitajika kutumia mashine hizo ni wale wafanyabiashara wenye mitaji kuanzia Mil 4 Tsh na kuendelea.
Wafanya biashara wamelalamika juu ya mfumo huo kutokana na gharama zinazotokana na mfumo huo,kwanza hizo mashine zinazofahamika kwa jina la ELECTRONIC FISCAL DEVICE(EFD) na inafahamika kwamba huuzwa kwa sh laki nane,hivyo si wote qambao wenye pesa kwa sasa kwa ajili ya kuknunua mashine hiyo,na kuzidi kuacha wafanya biashara kwenye mgomo mpaka sasa.
Vile vile wamelalamika juu ya makato yanayto tokana na matumizi ya mashine hiyo.Ambapo kila bidhaa inayotoka au risiti hukatwa asilimia 18.Kutokana na asilimia hiyo inayo katwa wafanya biashara wamelalamika kwamba ni kiasi kikubwa kulingana na kipato chao,kwanza asilimia kubwa ya bidhaa inatoka nje ya nchi,hivyo makato ama ushuru huanza kukatwa nje ya nchi,pili ikifika hapa nchini pia kuna ushuru unao katwa.Vile vile bado kodi nyingine kama za majengo ya biashara,umeme,malipo ya wafanyakazi usafiri n.k inachukua gharama kubwa kushinda faida au mapato wanayoyapata.
Licha ya hivyo wafanya biashara hao wamelalamika juu ya ongezeko la gharama ya umeme,majengo nayo ya biashara yamepanda bei,mishahara ya wafanya kazi naya imepanda n.k,hali hii hufanya wafanya biashara hawa wasione faida ya biashara zao.
Katika nyakati tofauti mwandishi wetu alibahatika kuongea na wafanya biashara mbalimbali wa kariakoo na kutoa maoni yao juu ya mgomo huu.Kwa kweli hali hii inatumiza sana,kul;ingana na gharama tunazolipa kwenye kodi zinaenda sawa na mtaji.Kwanza kuipatas mashine yenyewe shughuli,bila ya laki nane hupati,pili gharama inayokatwa katika kila risiti pia ni
kubwa kulingana na faida tunayoipata katika kila bidhaa.Alisema mfanya biashara mmoja jina hakulitaja.
Mfanya biashara mwengine aliyefahamika kwa jina la Bw Paul,alidai kuwa wao wanaonewa hususani wauza nguo amesema kuwa wamachinga au Panga boy wanawaumiza kiuchumi sababu wateja wengi hukimbia kununua bidhaa zao kutokana na ukubwa wa bei ukilinganisha bei wanazo uza wamachinga hao.Kwa kuwa wao hawalipi kodi hawaoni hasara nguo moja inayouzwa elfu thelathini kuuza elfu ishirini,hivyo hali hii inazidi kuwadidimiza kiuchumi,kwa kukosa wateja.
Wamachinga wananufaika sisi tunazidi kuathirika kutokana na ufinyu wa wateja,wingi wa ushuru,gharama zinazozidi kila siku n.k.Utakuta umetumia mtaji wa mil 10 na ukapata faida laki tano hapo bado vitu kibao unahitajika uvilipie,hivyo faida hakuna kabisa tunakuwa tunaifanyia kazi TRA na si kwa manufaa yetu.Kama sisi tunalazimishwa kutumia mashine hizo,basi hata wamachinga,mama lishe nao pia watumie siyo kutuonea sisi tu.Maana huenda wenzetu wanmapata faida zaidi yetu,ndiyo maana sasa wanafurahi kwa kuwa sisi tumefunga wao wanauza.je hiyo ni haki kweli?
Pia bado wizi nao unaofanyika kwa wabebaji,kwa aslimia kubwa ukiagiza mzigo lazima ujew nusu,utakuta wezi wanaiba na kwenda kuuza kwa bei za hasara wakati sisi tumezilipia kodi na kuzisafirisha kwa gharama kubwa sana mpaka zinafika hapa.
Pia wafanya biashara hao wameona bora waache kuuza kuliko kupoteza muda bure,alisema mfanyabiashara huyo,la sivyo haki itendeke kwa wote,na kusema kuwa wamachinga watanufaika kwa kutolipa kodi,na kupata wateja wengi,huku wao wakidorora na nguo zao hadi zipitwe na wakati hastimae kukosa wateja.Kama tunavyojua Watanzani ununua nguo ambazo matoleop ni mapya yakipitwa na wakati hayana soko tena.
Ukiangalia kwa asilimia kubwa sisi ni wachanga kibiashara,utakuta mtu ndiyo kwanza unaanza biashara,huku mtaji huenda ukawa umekopa,na kwa hali hii je tutapona kweli na kupata maendeleo? alisema mfanya biashara mwingine aliyefahamika kwa jina Bi Salma.
Hayo yalikuwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanya biashara wa Kariakoo.Juu ya utumiaji wa mashine inayofahamika kwa jina la ELECTRONIC FISCAL DEVICE.
Mgomo huu umesababisha wafanya biashara wengi wa kariakoo kama wamachinga,mamalishe,bodaboda,ingawa mgomo huu haukuwahusu pia walilalamika juu ya mgomo huu na kudai pia wamepata hasara kutokana nma ufinyu wea wateja.
Kwa kweli juzi nilimwaga ugali,mboga,na hata wali pia kwa sababu vilikosa walaji,tunategemea maduka makubwa yafunguliwe maana hao ndiyo wanaotuletea wateja,kama maduka yakifungwa ina maana na wateja hakuna wote wanalala majumbani kwao,alisema Bi Aisha mama ntilie wea vsokoni kariakoo mtaa wa kongo.
Nimepata hasara kweli,uchumi wangu umeshuka toka mgomo huu ulivyoanza juzi,mtaji nao umekatika naishia kukopa madukani.Kwa kweli huu mgomo ni majanga kwetu pia sio hao wafanya biashara wakubwa peke yao.Alisema Dada huyo
Ukweli ni kwamba ukiangalia jiji la Kariakoo toka jana halina mkusanyiko wa watu wengi.Na hata ukiangalia nyuso za wafanyabiashara zina huzuni wengine wana hasira juu ya jambo hili.
Hata wale waliotoka Mikoani pia wamelalamika kwa kukosa bidhaa kutokana na mgomo huo,na kudai kuwa wamepoteza nauli,muda,n.k,bila ya faida yoyote.
Hali hii ikiendelea wananchi wengi wataathirika kiuchumi,na kinachosikitisha kwamba wafanya biashara hao mpaka sasa hawajatoa tamko rasmi juu ya hatima ya mgomo huo na haijulikani utaisha lini.