DARREN BENT AINYIMA USHINDI MAN UNITED

BAO la dakika ya mwisho la Darren Bent limeinyima ushindi Manchester United baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 nyumbani Uwanja wa Old Trafford na Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Baada ya Fulham kupata bao la kuongoza kupitia kwa Steve Sidwell dakika ya 19, United ilipata mabao mawili ya haraka haraka na kuongoza mchezo kupitia kwa Robin van Persie dakika ya 79 na Michael Carrick 80.


Matokeo haya yanaifanya United ya David Moyes ijiongezee pointi moja na kufikisha 41 baada ya kucheza mechi 25, ikiendelea kubaki nafasi ya saba.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons