#MAONI: TFF IMEHODHI LIGI KWA AZAM
Na Prince Hoza KITENDO kilichofanywa na shirikisho la kandanda nchini TFF kuiruhusu Azam Fc kwenda Zambia kucheza mechi za kirafiki na kuikacha ligi kiu ya Vodacom Tanzania bata huku ikisababisha kupangua ratiba ya ligi hiyo si cha kuzoeleka hata siku moja. TFF imefanya kosa kubwa ambalo linaanza kuharibu sifa ya shirikisho hilo pamoja na Bodi yake ya ligi TPLB, Licha kwamba raisi wa shirikisho hilo Jamal Malinzi kuomba radhi lakini bado ni sawa na kazi bure, kwani kosa limeshafanyika. Bora ruhusa hiyo ingepewa Mwadui Fc au Kagera Sugar sidhani kama wadau wa soka wangelalamika sana, huenda wangelisifu shirikisho hilo kwani timu hizo hazipo kwenye mbio za ubingwa, kitendo cha kuiruhusu Azam Fc kinaonekana kama cha kuipendelea. Tunafahamu kwamba Azam Fc ni timu inayomilikiwa na bilionea Said Salim Bakhressa ambaye pia ndiye mmiliki wa Azam Tv yeye na familia yake. Azam Tv ni wadhamini wenza wa ligi kuu bara hivyo ina nguvu ndani ya shirikisho hilo, matajiri hao pia wanadhamini michu...