UCHAGUZI YANGA WANUKIA, SAM MAPANDE AWA MWENYEKITI WA KAMATI
Na Prince Hoza
UNAWEZA kusema sasa kimeeleweka. Uongozi wa mabingwa wa soka nchini Yanga Sc umemteua mwanasheria Sam Mapamde kuwa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro imedai kuwa Mapande anakuwa mwenyekiti wa kamati hiyo akichukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mwenyekiti wa kamati hiyo Alex Gaitani Mgongolwa.
Mgongolwa alijiuzuru wadhifa huo akidai ni kubanwa na majukumu ya kifamilia.
Yanga imetakiwa kufanya uchaguzi jana na raisi wa shirikisho la kandanda nchini TFF Jamal Malinzi.
Hata hivyo muda wa kukaa madarakani kwa viongozi wa klabu hiyo umekwisha kisheria.
Tayari mwenyekiti wa timu hiyo Yusuf Mehbood Manji ametangaza kutetea kiti chake, awali Manji aliwaomba Wanayanga kutowania tena kiti hicho na walimuongezea mwaka mmoja kuendelea kuiongoza, mwaka mmoja aliopewa imekwisha kisheria