HASSAN KESSY AIONGOZA SIMBA KUIUA AFRICAN SPORTS 4-0
Na Prince Hoza
Wekundu wa msimbazi Simba Sc jioni ya leo katika uwanja wa Taifa Dar es salaam imeishushia kipigo kitakatifu African Sports ya Tanga mabao 4-0 mchezo wa ligi kuu bara.
Chachu ya ushindi wa Simba katika mchezo wa leo ni beki wake wa upande wa kulia Hassan Ramadhan Kessy ambaye alicheza vizuri na kusaidia ushindi mnono wa timu hiyo ambayo imefikisha pointi 36.
Simba ilijipatia mabao yake matatu katika kipindi cha kwanza yakifungwa na Mganda Hamisi Kiiza "Diego" aliyetupia mawili na moja likifungwa na Kessy.
Kipindi cha pili Simba waliongeza juhudi na kupata bao la nne lililofungwa na mshambuliaji wake chipukizi Hajji Ugando