MBWANA SAMATTA KUCHEZA LIGI YA MABINGWA MSIMU UJAO
Na Alex Jonas
LEO klabu ya KRS Genk ya Ubelgiji inamtambulisha mchezaji wake mpya raia wa Tanzania Mbwana Ali Samatta.
Samatta aliondoka usiku wa kuamkia jana kuelekea jijini Brussers Ubelgiji kujiunga na timu yake mpya.
Mwanasoka huyo bora wa Afrika kwa wanaocheza ligi ya ndani, ameitwa kujiunga na timu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini humo akitokea TP Mazembe ya DRC ambapo aliiwezesha kutwaa ubingwa wa Afrika.
Kwa maana hiyo Samatta atacheza ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao kwani hadi sasa timu yake mpya ya Genk inaongoza ligi ya nchi hiyo