PETER MANYIKA AMSHANGAA MAYANJA KUMWEKA BENCHI

Na Mrisho Hassan

Mlinda mlango wa Simba Peter Manyika anaendelea kushangazwa na kitendo cha kocha wake Jackson Mayanja cha kumwanzishia benchi wakati bado kiwango chake ni cha juu.

Akizungumza na mwandishi wa blogu hii, Manyika alisema yeye bado kipa mahiri na anastahili kukaa langoni.

Anashangaa kuona anakalishwa benchi bila sababu yoyote, "Mimi ni kipa mahiri lakini sianzishwi katika kikosi cha kwanza, uwezo ninao ila ni matakwa ya kocha na wala siwezi kuamua", alisema.

Simba leo jioni inashuka katika uwanja wa Taifa kuvaana na African Sports ya Tanga uwanja wa Taifa Dar es salaam mchezo wa ligi kuu bara.

Tangia kumalizika kwa michuano ya kombe la Mapinduzi huko Zanzibar Simba ilikuwa ikimpanga golini Peter Manyika tena ikiwa chini ya kocha Muingereza Dylan Kerr ambaye baadaye akatimuliwa na kukabidhiwa jahazi Jackson Mayanja.

Hata hivyo Mayanja amekuwa akimtumia Vincent Angban

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA