COASTAL YAILOWESHA YANGA MKWAKWANI TANGA, AZAM MILANGO IKO WAZI KUSHIKA USUKANI
Na Alex Jonas
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Yanga Sc jioni ya leo katika uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga imekiona cha moto baada ya kulala mabao 2-0 na Coastal Union "Wagosi wa kaya".
Yanga leo imepotezwa kabisa na vijana wa Ally Jangalu na kujikuta inashindwa kuchomoza na ushindi kwenye mchezo huo.
Licha ya mchezo huo kutawaliwa na vurugu za hapa na pale zilizopelekea beki wa Yanga Kevin Yondan kupewa kadi nyekundu, magoli ya Wagosi wa kaya yaliwekwa kimiani na Miraji Adam na Juma Mahadhi.
Licha ya Yanga kulala mabao hayo mawili, Yanga inaendelea kuongoza ligi hiyo lakini imewapa nafasi kubwa Azam Fc kukamata usukani endapo itashinda mechi yake