KIONGERA BASI TENA, AFIKIRIA KUREJEA KWAO
Na Saida Fikiri
Hali si nzuri kwa kiungo mshambuliaji wa Simba Sc Paul Kiongera kufuatia mwenendo wake mbaya ndani ya klabu hiyo.
Simba ilifikia maamuzi ya kumrejesha mshambuliaji huyo baada ya kuridhishwa na kiwango chake alichokionyesha kwenye ligi kuu ya Kenya (KPL).
Mshambuliaji huyo aliyekuwa akiichezea timu ya KCB kwa mkopo aliibuka mfungaji bora kwenye ligi hiyo na ndipo Simba ilipoamua kumrejesha ikiamini atawasaidia.
Lakini hali iko tofauti kwani mchezaji huyo amezidi kushuka kiwango kila kukicha na tangia aanze kutumikia Simba hajafunga hata goli la kuotea.
Rafiki yake wa karibu ambaye naye ni raia wa Kenya ameitonya blogu hii kuwa mara baada ya kumalizika msimu huu jamaa anaweza kuchapa mwendo na kurejea kwao Kenya huku akiwa amekata tamaa