RASMI: SAMATTA ASAINI GENK MIAKA MINNE
Na Prince Hoza
Mtanzania Mbwana Samatta amesaini mkataba wa miaka minne kuanzia 2016 hadi 2020 kuitumikia timu yake mpya ya KRC Genk ya Ubelgiji.
Samatta amemalizana na vinara hao wa ligi kuu ya Ubelgiji na sasa si mchezaji wa TP Mazembe ya DRC ambapo aliiwezesha kutwaa ubingwa wa vilabu Afrika.
Mshambuliaji huyo aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani.
Bosi wa TP Mazembe Moise Katumbi amesaini fomu za kumuidhinisha mshambuliaji huyo aliyewahi kuzichezea Simba Sc, African Lyon na Kimbangulile zote za Tanzania