Machapisho

Simba nje Kagame Cup ikishinda 2-1

Picha
Timu ya Simba SC imefanikiwa kuambulia ushindi kwenye kombe la Kagame Cup baada ya kuifunga Singida Black Stars mabao 2-1 uwanja wa Amahoro jijini Kigali Rwanda. Mabao ya Simba yamefungwa na Ibrahim Doumbia dakika ya 27 na Elie Mpanzu dakika ya 66 wakati goli la Singida lilifungwa na Mathew Tegisia Momanyi dakika ya 55 na timu zote zimeaga mashindano hayo kufuatia pointi zao hazikuivuka Jamus ambayo imeingia nusu fainali kwa kufikisha pointi 7

Kocha wa Bafana Bafana ajiuzuru

Picha
Kocha Hugo Broos amejiuzulu nafasi ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) baada ya kuhudumu kwa miaka mitano!. Hugo amejiuzulu baada ya kumalizika kwa michuano ya FIFA World Cup 2026 na Afrika Kusini wapo wanatafuta mbadala wake mapema sana.

Fred Ngoma ni mwananchi

Picha
Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji namba 6, Fred Duval Ngoma, raia wa Jamhuri ya Congo Brazzaville, akitokea klabu ya Olympique de Safi inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco Botola Pro. Ngoma, mwenye umri wa miaka 28, anatajwa kuwa miongoni mwa viungo wenye uwezo mkubwa wa kucheza mbele ya safu ya ulinzi kutokana na uwezo wake wa kukaba, Mbali na nafasi yake ya kiungo mkabaji, pia ana uwezo wa kucheza kama kiungo wa kati pale inapohitajika. Katika msimu wa 2025,26 akiwa na Olympique de Safi, Ngoma alikuwa mchezaji muhimu wa kikosi hicho, akicheza mechi nyingi za ligi na kuonyesha kiwango cha juu cha uthabiti katikati ya uwanja. Kabla ya kutua Morocco, aliwahi kuzichezea klabu mbalimbali barani Afrika na pia amewahi kuitwa katika timu ya taifa ya Congo Brazzaville. Usajili wa Fred Ngoma unaonekana kuwa sehemu ya mkakati wa Yanga kuimarisha safu ya kiungo kuelekea msimu mpya wa mashindano ya ndani pamoja na michuano ya kimataifa.Ujio wake unatarajiwa kuongeza ushindani mkub...

Yanga na Simba kupigwa New Amaan Stadium

Picha
Mechi ya kuashiria kuanza Ligi Kuu ya NBC Primier League 2026/2027 Ngao ya Jamii inatarajia kuchezwa kwenye uwanja wa New Amaan Stadium mjini Zanzibar. Mechi hiyo iliyopangwa Agosti 12 mwaka huu inayokutanishwa watani wa jadi Yanga na Simba, itachezwa uwanja huo usiku saa 2' 30, Bodi ya Ligi wameelekeza mechi kufanyika Amaan Stadium badala ya uwanja wa Uhuru.

Nyota Yanga ateuliwa Rais wa klabu DR Congo

Picha
Aliyewahi kuwa mshambuliaji wa klabu ya Yanga SC, David Molinga 'Falcao' raia wa DR Congo, ameingia kwenye historia mpya katika maisha yake ya soka baada ya kuchaguliwa rasmi kuwa Rais wa Klabu ya AC Bandal kwa mkataba wa miaka mitano.  AC Bandal ni klabu yenye makao yake katika wilaya ya Bandalungwa mjini Kinshasa inayoshiriki Ligi ya EUFKIN-Malebo, na pia ni timu ambayo Molinga mwenyewe aliwahi kuitumikia zamani kama mchezaji. Kupitia ujumbe wake wa shukrani, Molinga amemshukuru Mwenyezi Mungu na kueleza fahari yake kubwa kupewa dhamana ya kuiongoza klabu hiyo iliyowahi kutwaa ubingwa wa Super Coupe ya Kinshasa mwaka 2014.  Amewaahidi wanachama, viongozi na mashabiki kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uwazi ili kuijenga AC Bandal kuwa klabu imara na yenye mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja. Uamuzi huu unamfanya 'Falcao' kujiunga na orodha ya wachezaji wa zamani barani Afrika waliofanikiwa kubadilisha viatu vya soka na kuvaa suti za uongozi katika ngazi ya juu y...

Barker aujia juu uongozi Simba, aponda usajili

Picha
Taarifa zinazoendelea kuzungumzwa ndani ya Simba SC zinaeleza kuwa kocha mkuu Steve Barker hakuwa ameridhishwa na baadhi ya usajili uliofanywa na klabu hiyo kuelekea msimu mpya. Inaelezwa kuwa Barker aliwasilisha mapendekezo yake ya wachezaji aliotaka kuimarisha kikosi, lakini si mapendekezo yote yaliyotekelezwa na uongozi. Kwa mujibu wa taarifa hizo, baadhi ya wachezaji waliosajiliwa hawakuwa sehemu ya chaguo la kwanza la kocha huyo. Majina yanayotajwa ni pamoja na mshambuliaji Doumbia, Chilambo na Jabaar, huku ikielezwa kuwa usajili wao ulifanyika kutokana na maamuzi ya uongozi badala ya mapendekezo ya benchi la ufundi. Aidha, Barker anaripotiwa kushangazwa na kushindwa kwa klabu kukamilisha baadhi ya mahitaji aliyoyaona kuwa ya msingi. Miongoni mwa hoja zinazotajwa ni kushindwa kufanikisha makubaliano yaliyohitaji malipo ya $50,000 kwa Wydad ili kuendelea na mchakato wa kumpata Selemani Gomez, jambo ambalo linaelezwa kuwa lilikuwa sehemu ya vipaumbele vyake katika kuimarisha kikosi...

Zougrana atambulishwa Yanga apewa jezi namba 6

Picha
Klabu ya Yanga SC imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kuimarisha kikosi kuelekea msimu mpya wa mashindano kwa kukamilisha usajili wa kiungo mahiri Mohamed Tchapi Zougrana, ambaye sasa amepatiwa jezi namba 6. Nyota huyu mwenye umri wa miaka 25 na raia wa Burkina Faso amejiunga na Wananchi akitokea MC Alger ya Algeria, baada ya awali pia kuitumikia ASEC Mimosas ya Ivory Coast. Zougrana anatambulika kwa uwezo wake wa kucheza nafasi ya kiungo wa kati kwa ustadi mkubwa. Ni mchezaji mwenye sifa ya kukaba kwa ufanisi, kumiliki mpira na kuanzisha mashambulizi kwa pasi sahihi. Uwezo huu unamfanya kuwa nyota wa kipekee ambaye anaweza kuimarisha safu ya kiungo ya Yanga SC na kuongeza ubunifu wa kikosi katika mechi ngumu. Jezi namba 6, ambayo mara nyingi huhusishwa na wachezaji wa kiungo wa kati wenye jukumu la kudhibiti mchezo, ni ishara ya imani kubwa ya klabu kwa uwezo wake.