Yanga yasaka saini ya Laurian Makame
YANGA wanapambana kuhakikisha wanatimiza matakwa ya kocha mkuu wa kikosi hicho, Sead Ramovic ambaye ameagiza kufanyika maboresho kadhaa katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo akitaja maeneo yanayotakiwa kuongezwa nguvu. . Kati ya maeneo hayo ni beki ya kushoto na kulia ambako tayari amesajiliwa Israel Mwenda kwa mkopo akitokea Singida Black Stars. Pia anahitajika beki wa kati, kiungo mkabaji, winga ya kushoto na mshambuliaji. . Katika kuanza na mikakati hiyo, haraka Mabosi wa Yanga wameamua kuhamishia nguvu kwa beki Mzenji, Laurian Makame anayeitumikia Fountain Gate. . Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga, kimeeleza kuwa viongozi wameweka nguvu Fountain Gate ili kumpata Makame ambaye amekuwa nguzo muhimu ndani ya kikosi hicho kilichoweka ngome yake Manyara ikiutumia Uwanja wa Tanzanite Kwaraa. Laurian Makame