Mapafu ya Mbwa kupanda ulingoni Desemba 26
Bondia wa Ngumi za Kulipwa hapa nchini Mfaume Ahmad Said a.k.a 'Mapafu Ya Mbwa' Tarehe 26/12/2024 anatarajia kucheza pambano la Kimataifa kwenye Mapambano ya 'Knockout Ya Mama 2.
Mfaume huyu ni bondia kutoka Gym la Naccoz liliopo maeneo ya Mabibo Makutano Dar es Salaam pia ni bingwa wa zamani aliyekuwa akishikilia Mikanda ya WBF African Super Welterweight kg 69 Title na mkanda wa East & Central Africa Super Welterweight kg 69 Title.
December 26 Mfaume ataenda kucheza pambano lake la kwanza kwa Mwaka huu baada ya kukaa mda mrefu bila kupigana mara ya Mwisho Mfaume kuonekana Ulingoni ilikuwa Tarehe 30/6/2023 ambapo alicheza dhidi ya bondia Chikondi Makawa raia wa Malawi pambano la Kimataifa la raundi 8 na alishinda kwa matokeo ya Point ya Majaji Wote Watatu.
Safari hii atakuwa na kibarua dhidi ya bondia Paulus Shishilven Amavila raia wa Namibia ambapo watacheza pambano la Kimataifa la raundi 8 lililo andaliwa na Mafia Boxing Promotion na litafanyika kwenye Ukumbi wa Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam.
Mpinzani wake Mfaume bondia Amavila huyu ni mzaliwa wa maeneo ya Onamanape japo kwa sasa ni mkazi wa maeneo ya Windhoek nchini Namibia safari yake ya mchezo wa Masumbwii kupitia Ngumi za Kulipwa ilianzia rasmii 24/11/2018.
Kwa kucheza pambano la raundi 4 dhidi ya bondia Emmanuel Jason raia wa Namibia na bondia Amavila alishinda pambano hilo kwa Matokeo ya Point ya Majaji wote Watatu.
Mpaka sasa ni bondia mwenye hadhii ya Nyota 1 na nusu anacheza kwenye uzani wa Welterweight kg 66 anashika Nafasi ya 264 / 2385 Duniani na Nafasi namba 4 / 18 kwa mabondia wote wanaocheza uzani huo wa kg 66 nchini kwao Namibia.
Akiwa na Rekodi ya Total Fight's 13, Win's 10, 'KO'S' 5, Lose 2 Draw 1.
Kwa upande wa Mfaume kutokana na kukaa mda bila kupigana rekodi yake kwa upande wa Hadhii na Nafasi imefungwa kwa mda (Inactive) na atakapo cheza pambano hili matokeo yake kiingizwa kwenye mtandao wa Boxrec rekodi yake kwa upande wa Hadhii na Nafasi itafunguliwa na kusoma rasmii.
Rekodi yake kwenye mapambano aliyocheza ana Total Fight's 28 Win's 18, 'KO'S' 8, Lose 8 Draw 2.
Tunamtakia kila kheri na maandalizi mema bondia Mfaume Mfaume kuelekea kwenye pambano hilo la Kimataifa.
