Machapisho

KESSY AIPA POINTI TATU MUHIMU YANGA DHIDI YA NDANDA

Picha
Na Ikram Khamees. Mtwara Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga Sc jioni ya leo imezidi kumfukuzia mtani wake wa jadi Simba kileleni, baada ya kuilaza Ndanda Fc mabao 2-1, mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Kwa ushindi huo sasa Yanga inafikisha pointi 40 ikiwa imeshuka dimbani mara 19 sawa na mahasimu wao Simba ambao wao wanaongoza ligi wakiwa na pointi 45, Yanga walianza kuhesabu bao la kwanza dakika ya 6 likifungwa na Pius Buswita akipokea pasi ya Hassan Kessy. Kabla ya mapumziko Hassan Kessy ambaye leo tena amekuwa lulu, aliifungia Yanga bao la pili na la ushindi, dakika ya 36  hata hivyo Yanga itajilaumu yenyewe kwa kukosa penalti iliyopigwa na Papy Kabamba Tshishimbi. Kipindi cha pili Ndanda nao walijipatia bao la kufuta machozi lililofungwa na Nassoro Kapama dakika ya 46 aliyepokea pasi ya Mrisho Ngasa "Anko", Yanga sasa wanarejea Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wao wa Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswa...

JERRY MURO: CHIRWA SI WA KUMLINGANISHA NA OKWI KWA SASA, OKWI MTU MWINGINE BWANA!

Picha
Na Mwandishi Wetu Aliyewahi kuwa Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Jerry Muro, ameeleza mtazamo wake wa kuwa nani anaweza kuwa mfungaji bora katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara. Muro amesema anampa nafasi kubwa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, kutokana na kiwango kizuri ambacho amekuwa akikionesha akiwa na Simba. Mbali na hilo, Muro pia amemtaja mchezaji wa Yanga, Obrey Chirwa kuwa hawezi kumfikia Okwi, kwani kiwango chake si kama cha mwenzake. Muro amesema Chirwa amekuwa akigoma kila wakati kuichezea hata timu yake, hivyo hampi na nafasi ya kuchuana na Okwi na akaenda mbali kwa kusema hastahili kulinganishwa naye. "Kwangu mimi Okwi ndiye mchezaji bora kwa sasa, hauwezi ukamlinganisha na Chirwa ambaye amekuwa akigoma hata kuichezea Yanga, Okwi ni ''Real Proffesional" hivyo hawezi kufikiwa na Chirwa katika mbio za ufungaji bora" alisema Muro. Okwi mpaka sasa amefikisha mabao 16 katika mechi 19 alizocheza msimu huu, wakati Chirwa ana mabao 11.  Emmanuel O...

BODI YA LIGI YANYOOSHA MIKONO KWA YANGA

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Hatimaye Bodi ya Ligi (TPLB) imeridhia klabu ya Yanga iendelee na maandalizi ya mchezo wake wa Ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuisogeza mbele mechi yake dhidi ya Mtibwa Sugar iliyokuwa ichezwe Jumamosi ijayo ya Machi 3 uwanja wa Jamhuri Morogoro wa Ligi Kuu Bara huku ikishuka tena uwanjani Machi 6 kucheza na Township Rollers ya Botswana. Yanga iliiomba Bodi ya Ligi kusogeza mbele mchezo wake angalau mmoja ili kuwapa nafasi ya kushiriki kikamilifu michuano ya kimataifa, mabingwa hao kupitia katibu wao mkuu, Charles Boniface Mkwasa walikuwa wakilalamikia ufinyu wa ratiba yao. Yanga ilipangiwa mechi zake mfululizo, Jumapili ilucheza na Majimaji ya Songea mchezo uliofanyika Songea wa hatua ya 16 Bora kombe la Azam Sports Federation Cup, lakini pia ikapangiwa kucheza na Ndanda Jumatano kabla tena Jumamosi kupangwa kucheza na Mtibwa Sugar. Lakini Bodi ya Ligi imeamua kusogeza mbele mchezo wao wa VPL dhidi ya Mtibwa Sugar ambao ilikuwa uchezwe Juma...

SIMBA KANYAGA TWENDE HADI UBINGWA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba Sc, jioni ya leo wameendeleza ubabe wao baada ya kuichapa bila huruma Mbao Fc ya Mwanza mabao 5-0 uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Mbao Fc walionekana kuibana Simba dakika 20 za mwanzo wa mchezo lakini kocha wa Simba aliona udhaifu wa Simba na kuamua kumwingiza kiungo Mzamiru Yassin ambaye akaubadili mchezo na Simba kuanza kujipatia mabao mawili hadi mapumziko. Shiza Kichuya alianza kufunga dakika ya 38 kabla ya Emmanuel Okwi ajaongeza la pili dakika ya 41, kipindi cha pili Okwi tena akafunga la tatu dakika ya 68 wakati Erasto Nyoni akafunga la nne na Mghana, Nicolaus Gyan alihitimisha kalamu ya magoli kwa kufunga dakika ya 86. Kwa matokeo hayo Simba wanafikisha pointi 45 wakiendelea kuongoza na sasa ikitanua gepu kubwa na mahasimu wao Yanga ambao wanafuatia kwa kushika nafasi ya pili, Yanga ina pointi 37 ikiachwa nyuma kwa pointi 7 Simba imeifunga Mbao mabao 5-0

SUGU AHUKUMIWA MIEZI 5 JELA KWA KUMTUSI RAIS MAGUFULI

Picha
Na Exipeditor Mataruma. Mbeya Mbunge wa Mbeya mjini na mwanamuziki maarufu wa Hip Hop hapa nchini, Joseph Osmund Mbilinyi, amehukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kwa kosa la kumtukana Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Dk John Joseph Pombe Magufuli. Hakimu mkazi wa mahakama ya Mbeya mjini, Michael Mteite ametoa hukumu hiyo leo baada ya kujiridhisha kuwa Sugu ambaye ni mbunge wa jimbo la Mbeya kumtusi Rais wa nchi jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Mteite ametoa hukumu hiyo ili wabunge na watu wengine wasifanye hivyo kwani ni kosa kubwa kutoa lugha chafu kwa mtu mwingine pia kwa Rais wa nchi, licha ya Sugu kuhukumiwa miezi mitano, mahakama hiyo imemuhumu katibu wa chama hicho mkoani Mbeya, Emmanuel Masonga miezi sita naye akihusika kumtusi Rais Magufuli Joseph Mbilinyi amehukumiwa jela miezi kwa kumtukana Rais Magufuli

Kispoti

Picha
Yanga wapo katika wakati mgumu lakini........ Na Prince Hoza TANGU alipojiondoa Yusuf Mehbood Manji ambaye alikuwa mwenyekiti na mfadhili wa klabu ya Yanga morali imeshuka, fedha imetoweka hata kasi ya timu inaonekana kupungua. Uwepo wa Manji ndani ya Yanga uliwapa faida kubwa Wanayanga, Yanga imetawala soka la Tanzania takribani miaka mitano, huku ikiwateza mahasimu wao Simba Sc ambao ilifikia wakati ilipachikwa jina la utani la "Wamchangani" jina ambalo walibatizwa na aliyekuwa msemaji wa Yanga, Jerry Muro. Jerry Muro akaendelea kuibatiza majina mengine ya utani Simba na kuwakera mashabiki wake, Simba iliitwa "Wamatopeni" na hiyo yote ni kutokana na matokeo mabovu iliyopata. Uwepo wa Manji uliwafanya wachezaji wa Yanga waishi kifalme, Yanga iliweza kusajili wachezaji bora kutoka kila mahari, na ndio maana ikaweza kujiwekea historia ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mara tatu mfululizo. Manji akaipoteza kabisa Simba ambayo ilishindwa kufu...

Matokeo yoote kombe la Azam Sports Federation Cup

Picha
Mzunguko wa 4 wa michuano ya Azam Sports Federation Cup unaelekea kukamilika kesho Februali 25, 2018 na timu nane zitasalia kucheza robo fainali. Angalia matokeo yote na ratiba iliyobaki ya mechi mbili zitakazopigwa, Mwandishi wetu, Salum Fikiri Jr anatupasha. Njombe Mji 1 Mbao Fc1 (Penalti 6-5), Singida United 2 Polisi Tanzania 0, Azam Fc 3 KMC 1, Yanga 2 Majimaji 1, Mtibwa Sugar 3 Buseresere 0, JKT Tanzania 1 Ndanda Fc 0, leo ni Stand United va Dodoma Fc, CCM Kambarage na Kiluvya United vs Tanzania Prisons, Filbert Bayi Stadium, Kibaha Azam Fc imekata tiketi ya robo fainali ya michuano hiyo