SUGU AHUKUMIWA MIEZI 5 JELA KWA KUMTUSI RAIS MAGUFULI
Na Exipeditor Mataruma. Mbeya
Mbunge wa Mbeya mjini na mwanamuziki maarufu wa Hip Hop hapa nchini, Joseph Osmund Mbilinyi, amehukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kwa kosa la kumtukana Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Dk John Joseph Pombe Magufuli.
Hakimu mkazi wa mahakama ya Mbeya mjini, Michael Mteite ametoa hukumu hiyo leo baada ya kujiridhisha kuwa Sugu ambaye ni mbunge wa jimbo la Mbeya kumtusi Rais wa nchi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Mteite ametoa hukumu hiyo ili wabunge na watu wengine wasifanye hivyo kwani ni kosa kubwa kutoa lugha chafu kwa mtu mwingine pia kwa Rais wa nchi, licha ya Sugu kuhukumiwa miezi mitano, mahakama hiyo imemuhumu katibu wa chama hicho mkoani Mbeya, Emmanuel Masonga miezi sita naye akihusika kumtusi Rais Magufuli