BODI YA LIGI YANYOOSHA MIKONO KWA YANGA
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Hatimaye Bodi ya Ligi (TPLB) imeridhia klabu ya Yanga iendelee na maandalizi ya mchezo wake wa Ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuisogeza mbele mechi yake dhidi ya Mtibwa Sugar iliyokuwa ichezwe Jumamosi ijayo ya Machi 3 uwanja wa Jamhuri Morogoro wa Ligi Kuu Bara huku ikishuka tena uwanjani Machi 6 kucheza na Township Rollers ya Botswana.
Yanga iliiomba Bodi ya Ligi kusogeza mbele mchezo wake angalau mmoja ili kuwapa nafasi ya kushiriki kikamilifu michuano ya kimataifa, mabingwa hao kupitia katibu wao mkuu, Charles Boniface Mkwasa walikuwa wakilalamikia ufinyu wa ratiba yao.
Yanga ilipangiwa mechi zake mfululizo, Jumapili ilucheza na Majimaji ya Songea mchezo uliofanyika Songea wa hatua ya 16 Bora kombe la Azam Sports Federation Cup, lakini pia ikapangiwa kucheza na Ndanda Jumatano kabla tena Jumamosi kupangwa kucheza na Mtibwa Sugar.
Lakini Bodi ya Ligi imeamua kusogeza mbele mchezo wao wa VPL dhidi ya Mtibwa Sugar ambao ilikuwa uchezwe Jumamosi na sasa itapata muda wa kujiandaa