KESSY AIPA POINTI TATU MUHIMU YANGA DHIDI YA NDANDA

Na Ikram Khamees. Mtwara

Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga Sc jioni ya leo imezidi kumfukuzia mtani wake wa jadi Simba kileleni, baada ya kuilaza Ndanda Fc mabao 2-1, mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Kwa ushindi huo sasa Yanga inafikisha pointi 40 ikiwa imeshuka dimbani mara 19 sawa na mahasimu wao Simba ambao wao wanaongoza ligi wakiwa na pointi 45, Yanga walianza kuhesabu bao la kwanza dakika ya 6 likifungwa na Pius Buswita akipokea pasi ya Hassan Kessy.

Kabla ya mapumziko Hassan Kessy ambaye leo tena amekuwa lulu, aliifungia Yanga bao la pili na la ushindi, dakika ya 36  hata hivyo Yanga itajilaumu yenyewe kwa kukosa penalti iliyopigwa na Papy Kabamba Tshishimbi.

Kipindi cha pili Ndanda nao walijipatia bao la kufuta machozi lililofungwa na Nassoro Kapama dakika ya 46 aliyepokea pasi ya Mrisho Ngasa "Anko", Yanga sasa wanarejea Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wao wa Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana, Machi 6 mwaka huu

Hassan Kessy ameipa Yanga pointi tatu leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA