AZAM FC KUISHUSHA SIMBA KILELENI LEO?
Na Exipeditor Mataruma. Mbeya Mabingwa wa kombe la Mapinduzi, Azam Fc leo inashuka uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya kuumana na wenyeji wanajeshi wa magereza Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Azam Fc ambayo Alhamis iliyopita ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Majimaji Fc uwanja wa Majimaji mjini Songea, inahitaji ushindi katika mchezo wa leo ili iweze kuishusha kileleni Simba kwani mpaka sasa ina pointi 27 na ikishinda itakuwa na 30. Lakini siyo kazi rahisi kuishinda timu hiyo inayokamata nafasi ya sita ikiwa na pointi 21 kwani timu hiyo ina kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mbeya City uwanja wa Sokoine, Mbeya. Mechi nyingine zitakazopigwa leo ni Mbao Fc na Stand United, CCM Kirumba Mwanza, Mtibwa Sugar na Njombe Mji, Manungu Complex , Morogoro na Mwadui Fc na Ndanda Fc, Mwadui Complex, Shinyanga Azam Fc inacheza na Prisons leo