DALALI KUZUNGUKA NCHI NZIMA KUHAMASISHA UBINGWA WA VPL

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Mwenyekiti wa zamani wa vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba Sc, Hassan Dalali "Field Marshal" ameamua kuzunguka karibu mikoa saba nchini kuwahamasisha Wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuisapoti kwa nguvu zao ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza jana mara baada ya Simba kuibugiza Singida United mabao 4-0, Dalali amesema anajisikia furaha kwa ushindi huo na anawataka Wanasimba kuungana kuhakikisha Simba inachukua ubingwa wa Bara.

Simba ina kiu ya ubingwa baada ya kucheza misimu mitano pasipo kupata ubingwa huku watani zake Yanga na Azam wakipokezana utawala wa soka, lakini msimu huu amedai iwe isiwe lazima wachukue ubingwa.

Simba inaongoza Ligi ikiwa na pointi 29 ikicheza mechi 13 ikifuatiwa na Azam Fc yenye pointi 27, mahasimu wao Yanga wenyewe wameachwa mbali kwani wana pointi 22 wakishika nafasi ya tano

Mikoa ambayo ametaja kwenda ni Morogoro, Tanga, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Iringa, Songea, Kagera na Zanzibar.

Hassan Dalali (Kulia) anatazamiwa kuhamasisha Wanasimba wote nchini Simba kutwaa VPL

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons