LIPULI YAIKABA KOO MBEYA CITY, NYUMBANI

Na Exipeditor Mataruma. Mbeya

Timu ya Lipuli Fc ya Iringa jioni ya leo imeikaba koo Mbeya City baada ya kuilazimisha sare tasa 0-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Vijana wa Mbeya City ambao sasa ni kama yatima baada ya kutemwa na wamiliki wake Halmashauri ya jiji la Mbeya MCC, imejikuta ikishindwa kupata ushindi nyumbani.

Kwa matokeo hayo Mbeya City imefikisha pointi 13 na mechi 13 huku Lipuli ikifikisha pointi 15 na mechi 13, ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa mechi nne, Mbao Fc itaialika Stand United, CCM Kirumba, Mtibwa Sugar na Njombe Mji, Manungu Complex Prisons na Azam Fc, Azam Complex, Chamazi na Mwadui itaumana na Ndanda Fc, Mwadui Complex, Shinyanga

Lipuli Fc imeibana koo Mbeya City

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons