Machapisho

MICHAEL WAMBURA NAYE ACHUKUA FOMU YA URAIS SIMBA, SASA NI VITA NA EVANS AVEVA

Picha
BAADA ya ‘memba’ wa kundi la Friends Of Simba (F.O.S), Evans Elieza Aveva jana kuchukua fomu ya kugombea Uenyekiti wa Simba SC, hasimu mkubwa wa kundi hilo, ‘Komredi’ Michael Richard Wambura naye leo amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo. Wambura anayefanya idadi ya wagombea Urais wa Simba SC kufika watatu baada ya Aveva na Andrew Tupa, alifika makao makuu ya klabu majira ya saa tano na ushei asubuhi ya leo akisindikizwa na wafuasi wake, na kwenda kuchukua fomu hiyo. Wambura hakwenda kwa mbwembwe nyingi na msafara mkubwa kama ule uliomsindikiza Aveva jana na baada ya kuchukua fomu aliondoka zake. Wambura ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Muda Simba SC mwaka 2006, ameingia na sera za kuinua uchumi wa klabu na kuboresha timu.

BRENDAN RODGERS KUONGEZA WAPYA LIVERPOOL, ATAMBA KUREJEA NA KASI YA UBINGWA MSIMU UJAO

Picha
KOCHA wa Liverpool,  Brendan Rodgers ameumia sana baada ya kikosi chake kushika nafasi ya pili katika mbio za ubingwa wa ligi kuu soka nchini England, lakini amesisitiza kuwa timu yake itarejea kushindana tena msimu ujao. Mabao ya Daniel Agger na Daniel Sturridge  yaliipa ushindi wa mabao 2-1 Liverpool dhidi ya Newcastle, lakini bao la wapinzani hao wa majogoo wa jiji lilitokana na Martin Skrtel kujifunga mwenyewe na likiwa ni bao la nne la kujifunga msimu huu. Licha ya Liverpool kushinda, Anfield ilikuwa kimya baada ya Man City kushinda mabao 2-0 dhidi ya West Ham na kutwaa ubingwa wa pili ndani ya misimu mitatu.Rodgers aliwaambia Sky Sports: ‘Tulicheza vizuri sana lakini hatukuweza kupata matokeo ya kuridhisha”.

HENRY JOSEPH AACHANA RASMI NA SIMBA, AKARIBISHA DILI MPYA

Picha
NAHODHA wa zamani wa Taifa stars na kiungo wa Simba sc msimu uliopita, Henry Joseph Shindika amesema kwa sasa ni mchezaji huru na anakaribisha klabu yoyote kufanya mazungumzo. Katika mahojiano maalum na mtandao huu, Joseph amesema bado anahitaji kucheza soka nchini Tanzania, japokuwa kuna mchakato anaufanya na kama atafanikiwa anaweza kwenda nje ya nchi. “Nimemaliza mkataba Simba, naweza kucheza klabu yoyote ya hapa nyumbani, cha msingi ni kuzungumza juu ya maslahi”. Joseph alisema Simba sc hawajazungumza na yeye kuhusu kuongezewa mkataba, hivyo timu yoyote itakayokaa mezani na kuelewana, atafanya kazi bila tatizo lolote.

JAVIER ZANETTI ATHIBITISHA KUSTAAFU

Picha
Javier Zanetti Mkabaji kamili wa Inter Milan na Argentina Javier Zanetti alithibitisha Jumanne kwamba atastaafu mwishoni mwa msimu baada ya kucheza mechi 800 kwenye misimu 19 akiwa na klabu hiyo ya Serie A. “Nilihisi kwamba wakati umefika,” Zanetti, anayetimiza miaka 41 Agosti na anayesifiwa sana kwamba mchezaji wa kuigwa, aliambia gazeti la Buenos Aires la La Nacion kwenye mahojiano. “Soka imenipa mengi sana na nimefurahia yote.” Zanetti, aliyechezea taifa lake mechi 145 licha ya kuachwa nje ya vikosi vya Kombe la Dunia 2006 na 2010 katika hali ya kutatanisha, alijeruhiwa misuli ya kigundo cha mguu Aprili, jeraha lake la kwanza kuu katika uchezaji wake. Alipona na kurudi tena uwanjani na kucheza mechi 10 katika Serie A msimu huu.

MAN CITY YANUSA UBINGWA ENGLAND

Picha
Man City wanaelekea kileleni mwa ubingwa wa ligi ya Uingereza Ilitarajiwa kwamba Manchester City itapiga hatua, lakini kwa mabao 4 - 0 dhidi ya Aston Villa, ilikuwa kweli mavuno yaliyowarejesha watakapo - kileleni na kuelekea ushindi wa dhahiri wa ligi ya England.

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KWANZA KUFUNZA SOKA LA WANAUME DUNIANI

Picha
Helena Costa kocha mpya wa timu ya Clermont ya Ufaransa Helena Costa raia wa Ureno atakuwa mwanamke wa kwanza kuwa kocha wa timu ya kulipwa ya wanaume nchini Ufaransa baada ya kutangazwa na timu ya Clermont Foot 63 kuwa kocha wake mkuu, Jumatano.

OWEN KASULE AKARIBIA SIMBA, HANSPOPPE ATANGAZA KUCHUKUA WANAOTEMWA NA AZAM

Picha
Klabu ya Simba inamfukuzia mfungaji bora wa michuano ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu, Mganda Owen Kasule wa URA ya Uganda ili akipige kwenye timu hiyo msimu ujao. Habari za uhakika kutoka kwa kiongozi  wa juu wa klabu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi zilisema kuwa Simba wako kwenye hatua za mwisho za kumalizana na kiungo mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda. Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hanspope  hakutaka kukubali wala kukanusha habari hizo. “Usajili tutafanya. Kuna wachezaji ambao bado tunazungumza nao, na tunafanya kwa taratibu hatutaki kutangaza mambo yetu, ukitangaza tu basi hapo hapo na Yanga wanakimbilia kumsajili,” alisema Hanspope.