BRENDAN RODGERS KUONGEZA WAPYA LIVERPOOL, ATAMBA KUREJEA NA KASI YA UBINGWA MSIMU UJAO

KOCHA wa Liverpool,  Brendan Rodgers ameumia sana baada ya kikosi chake kushika nafasi ya pili katika mbio za ubingwa wa ligi kuu soka nchini England, lakini amesisitiza kuwa timu yake itarejea kushindana tena msimu ujao.

Mabao ya Daniel Agger na Daniel Sturridge  yaliipa ushindi wa mabao 2-1 Liverpool dhidi ya Newcastle, lakini bao la wapinzani hao wa majogoo wa jiji lilitokana na Martin Skrtel kujifunga mwenyewe na likiwa ni bao la nne la kujifunga msimu huu.

Licha ya Liverpool kushinda, Anfield ilikuwa kimya baada ya Man City kushinda mabao 2-0 dhidi ya West Ham na kutwaa ubingwa wa pili ndani ya misimu mitatu.Rodgers aliwaambia Sky Sports: ‘Tulicheza vizuri sana lakini hatukuweza kupata matokeo ya kuridhisha”.

“Wachezaji wamekuwa katika kiwango cha juu, kushinda mechi 12 kati ya 14 inaonesha kuwa klabu ina kundi la watu linaloweza kufanya vizuri msimu ujao.

Tutajifunza kwa kila kosa tulilofanya msimu huu na kujiandaa kwa msimu ujao”.
Alipoulizwa kama klabu yake inaweza kupambana kwa kasi ile ile msimu ujao, Rodgers alisema: “Ndiyo. Tumeshika nafasi ya pili mbele ya timu imara.

Hongera kwa Manchester City, wameshinda taji wakiwa na kocha mzuri na kikosi cha wachezajii bora duniani, nawapongeza sana”.

“Tumepambana mpaka mchezo wa mwisho. Hii ni timu iliyoshika nafasi ya sabu mwaka jana.
“Tunajua tutakuwa bora zaidi kwasababu tutaboresha kikosi na tutaendelea kujiimarisha zaidi”.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons