HUYU NDIYE MWANAMKE WA KWANZA KUFUNZA SOKA LA WANAUME DUNIANI
Helena Costa kocha mpya wa timu ya Clermont ya Ufaransa
Helena Costa raia wa Ureno
atakuwa mwanamke wa kwanza kuwa kocha wa timu ya kulipwa ya wanaume
nchini Ufaransa baada ya kutangazwa na timu ya Clermont Foot 63 kuwa
kocha wake mkuu, Jumatano.
Klabu ya Clermont ya Ufaransa
Clermont inashika nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligue 2 nchini Ufaransa ikibakia michezo miwili kukamilisha msimu wa ligi hiyo.
Clermont itawategemea wachezaji 17 ambao kwa sasa bado wana mikataba na itawaongeza wachezaji chipukizi kutoka timu hiyo.
Olivier Chavanon, amekuwa na uzoefu mkubwa na uelewa wake wa kina wa timu hiyo utasaidia kuwa karibu zaidi mchezoni.
Utambulisho wa meneja mpya wa timu ya Clermont utafanyika Clermont-Ferrand mwisho mwa msimu wa 2013/2014.