MPIRA PESA WAMSHIKA PABAYA RAGE, BI HINDU AGONGELEA MSUMARI WA MOTO
KUNDI la wanachama wa Simba maarufu kabisa kama Mpira Pesa lenye maskani yake Magomeni Mikumi jijini limemjia juu mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaj Ismail Aden Rage (Pichani) kutokana na matamshi aliyoyatoa wakati wa mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika jumamosi iliyopita kwenye bwalo la maafisa wa polisi Osterbay.