NGUMI AFRIKA KUMKUTANISHA MTAGWA NA BFT
Shirikisho la ngumi za ridhaa nchini (BFT) linatarajia kutumia muda wa
mashindano ya ngumi ya nchi za Afrika yatakayofanyika nchini Mauritius
kuanzia Septemba mosi hadi 7 kumuona bondia Petro Mtagwa ambaye
anataumikia kifungo nchini humo.
Mtagwa alihukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani hivi karibuni nchini humo kutokana na hatia ya kuingiza dawa za kulevya wakati alipokwenda nchini humo katika mashindano ya kujipima nguvu.
Akizungumza jana, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga (Pichani) alisema tayari shirikisho limethibitisha ushiriki wake katika mashidano hayo ya kutafuta nafasi ya kushiriki kwenye michezo ya Jumuiya Madola.
Mashaga alisema wao kama shirikisho watatumia nafasi hiyo, kama sheria za nchi hiyo zitawaruhusu, kumuona na kuzungumza naye Mtagwa gerezani, wakati wakiwa katika mashindano hayo yanayoshirikisha timu za mataifa ya Afrika.
Alifafanua kuwa katika safari yao watakuwa na jumla ya mabondia 10, kocha wa timu, kiongozi wa shirikisho na kiongozi kutoka serikalini atakayeteuliwa kuongozana na timu hiyo.
Alisema pia wanatoa nafasi ya ziada kwa wadau wanaotaka kwenda na timu hiyo kwa ajili ya kwenda kuishangilia wakati wa mashindano.
Alisema kutokana na hilo wadau wote wa ngumi na wale wenye mapenzi mema na mchezo wa ngumi wanapaswa kujitokeza mapema ili kupewa taratibu za kwenda nchini humo.