Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2015

MWADUI FC YA JULIO YADAI ITAKUWA TIMU YA KWANZA KUIFUNGA YANGA KESHO

Picha
Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema wao ndiyo watakuwa wa kwanza kuitandika Yanga. Mwadui FC ya mkoani Shinyanga inaikaribisha Yanga mjini humo keshokutwa Jumatano katika mechi ya Ligi Kuu Bara. Julio amesema Mwadui FC itakuwa ya kwanza kuifunga Yanga ambayo imecheza mechi mfululizo bila ya kufungwa. “Timu yetu ilianza kwa kuonekana haifai, ilidharauliwa na wengi walisema ni timu ya wageni.

MOURINHO ASHITAKIWA KWA UTOVU WA NIDHAMU

Picha
Jose Mourinho amefunguliwa mashtaka ya utovu wa nidhamu na Shirikisho la Soka la Uingereza kwa sababu ya lugha aliyoitumia na vitendo vyake wakati wa mechi ambayo Chelsea walichapwa na West Ham United wikendi. Mourinho alifukuzwa eneo la marefa uwanjani baada yake kwenda kutaka kuzungumza na refa Jon Moss katika chumba chake wakati wa mapumziko mechi hiyo ya Jumamosi. Klabu zote mbili pia zimeshtakiwa kwa kushindwa kudhibiti wachezaji na zimepewa hadi Oktoba 29 kujibu mashtaka hayo. Chelsea tayari wanakabiliwa na faini ya £25,000 kwa wachezaji zaidi ya watano kupewa kadi za manjano wakati wa mechi hiyo ya Ligi ya Premia.

KOCHA TOTO AFRICANS AACHIA NGAZI, NI YULE MJERUMANI, NJAA YATAJWA

Picha
KOCHA Mjerumani wa Toto Africans ya Mwanza, Martin Grelis ameachia ngazi katika timu hiyo, akitoa sababu zaidi ya tatu, kubwa ni wachezaji kutothaminiwa na uongozi mbovu wa timu. Grelis aliyeanza kazi Julai mwaka huu, amesema kwamba ameamua kuacha kazi baada ya kugundua hata wachezaji hawalipwi mishahara. Aidha, safari za ‘kigumu’ kwenda mikoa ya Tanga na Tabora katika mechi zao za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara nazo zimechangia kumfanya aachie ngazi, ingawa mwenendo wa timu si mbaya hadi sasa. “Kwa mwezi mzima tumefanya mazoezi ya uhakika mara saba tu, hali ambayo kocha yeyote hawezi kukubaliana nayo, nami kama kocha, imenilazimu kuchukua uamuzi huu ambao ungechukuliwa na kocha yeyote,”amesema.

KERR AUCHIMBA MKWARA UONGOZI WA SIMBA, ADAI HAUNA UBAVU WA KUVUNJA MKATABA

Picha
Kocha wa Simba, Dylan Kerr amehoji sababu za uongozi wa klabu hiyo kumpa kipimo cha mechi mbili ili afahamu kama atabaki Msimbazi au anaondoka. Kocha Kerr ameukosoa uamuzi huo akisema, kinachokusudiwa kufanywa uongozi wake, hakikubaliki kwa mujibu wa mkataba walioingia. Uongozi wa Simba umemtaka  kocha huyo raia wa Uingereza kuhakikisha anapata ushindi katika mechi mbili kwenye ratiba ijayo dhidi ya Coastal Union ya Tanga na Majimaji ya Songea. Akizungumza na gazeti hili jana jijini, Kerr, alisema uamuzi wowote wa kumtimua baada ya mechi hizo mbili ni kinyume na makubaliano. Kerr alisema mkataba alioingia na Simba ni kuhakikisha timu hiyo inamaliza msimu na kushika moja ya nafasi mbili za juu. "Najua siku moja nitaondoka Simba, lakini kwa sasa wakifanya hivi watakuwa wamekosea sana, kama kipimo ni kuangalia nafasi ya timu kwenye msimamo, hawako sahihi. Timu zilizo juu yetu tumetofautiana pointi nne, si nyingi na wakumbuke Simba imecheza mechi ngumu ugenini, wakati A...

NEW CASTLE YAINYUKA NORWICH CITY

Picha
Ligi kuu ya soka ya England ilieendelea tena hapo jana kwa mchezo mmoja ambapo New castle United walikuwa wenyeji wa Norwich city katika dimba la St James' Park. Katika mchezo huo New castle waliibuka na ushindi mnono wa mabao 6-2, ambapo karamu ya mabao hayo ilihitiishwa na mchezaji Mitrovic dakika ya 64 kipindi cha pili. Kwa matokeo hayo yanaifanya New castle kukaa katika nafasi ya 18 ikiwa na pointi 6, na huo ni ushindi wa kwanza kwa Timu hiyo tangu msimu huu uanze ikiwa imecheza mechi tisa mpaka sasa, imedroo mechi 3, imepotezamichezo 5 na imejikusanyia jumla ya pointi 6 .

KERR ATAMBA KUENDELEZA UBABE MBEYA

Picha
Baada ya kuvunja mwiko wa kuwa kibonde wa Mbeya City katika misimu miwili iliyopita, benchi la ufundi la Simba limetamba litaendeleza kaulimbiu ya 'mabadiliko' inayotamba nchini kwa sasa kwa kuibuka na ushindi dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya keshokutwa. Simba ililazimishwa sare na Mbeya City katika mechi zote mbili za msimu wa kwanza (2013/14) wa timu hiyo ya Mbeya kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), kabla ya kuchezea kichapo katika mechi zote mbili za msimu uliopita wa ligi hiyo, 2-1 nyumbani na 2-0 ugenini, lakini juzi Wanamsimbazi walianza na kikosi chenye viungo watano, Said Ndemla, Jonas Mkude, Abdi Banda, Mwinyi Kazimoto na  Justice Majabvi na kuchomoza na ushindi wa 1-0 dhidi ya

KIVUMBI LIGI KUU KUENDELEA JUMATANO, AZAM MGUU SAWA KUIKABILI NDANDA

Picha
KIKOSI cha Azam FC kinatarajiwa kuondoka kesho Dar es Salaam kwenda Mtwara kwa ajili ya mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Alhamisi dhidi ya wenyeji, Ndanda FC. Baada ya sare ya 1-1 na mabingwa watetezi, Yanga SC, Azam FC wamepania kufufua wimbi lao la ushindi keshokutwa mjini Mtwara. Azam FC ambao walilalamikia uchezeshaji mbovu wa refa Abadallah Kambuzi wa Shinyanga Jumamosi dhidi ya Yanga SC, wataendelea kumkosa kocha wao, Muingereza Stewart John Hall siku hiyo uwanjani kwa sababu bado anatumikia adhabu yake ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa katka mchezo dhdi ya Coastal Union. Stewart atasafiri na timu na kuiandaa kama kawaida mazoezini, lakini siku ya mechi atakuwa jukwaani na mashabiki wengine kuangalia mchezo. Azam FC inafukuzana na Yanga SC kileleni mwa Ligi Kuu, kila timu ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi sita, wakifuatiwa na Simba SC wenye pointi 15.

Lowassa aiteka Kusini

Picha
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akitangaza kuahirishwa mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa chama hicho anayeungwa mkono na vyama vya Ukawa Edward Lowassa kutokana na hitilafu ya mitambo ya vipaza sauti.   Mji wa Tunduma jana umelazimika kusimamisha shughuli zake kwa kufunga maduka, biashara na barabara baada ya umati wa wananchi wa mji huo kujitokeza kumpokea mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa. Baadhi ya wananchi walikesha kwenye viwanja vya Shule ya Msingi ya Tunduma, wakimsubiri mgombea huo kuwasili kwenye mji huo, uliopo wilayani Mbozi. Hata hivyo, kiu ya wananchi hao kumsikiliza mgombea hiyo haikumalizwa, baada ya mkutano wake kuahirishwa saa 11 jioni kutokana na tatizo la mitambo. Nipashe ilishuhudia maduka yakifungwa huku wengine wakisema wanaenda kumsikiliza rais wa nchi. “Hapa mambo yote ni Lowassa...leo hakuna kazi, hakuna biashara na wala hakuna kubadilisha pesa, mambo yote ni Lowa...

FREEMASON YAMTESA MKOLA MAN, WAZAZI WAKE WAMJIA JUU.

Picha
Kuhusishwa kwa msanii wa hip hop wa mkoani Tanga Mkola Man na dini ya kishetani ya Freemason kumewashitua wazazi wake ambapo wamemjia juu na kutaka awathibitishie nini anachotaka kuwafanyia mpaka kuingia kwenye imani hiyo mbaya. Wakizungumza na Mambo uwanjani, wazazi hao wamesema kuwa mtoto wao amejiunga kwenye dini hiyo ikiwa wao ni walokole, 'tunanyooshewa vidole na watu tunapokuwa kanisani na ikafikia hatua tukaanza kutengwa', walisema. Lakini wakadai walipopata ukweli kuwa mtoto wao (Mkola Man) ni freemason wakamtaka aeleze ukweli iweje ajiunge na dini hiyo, akiwajibu wazazi wake, Mkola Man alisema yeye si freemason ila aliamua kujiita hivyo ili ajulikane.

MAKALA: SIMBA ILIPOTEA MABOYA KWA ANGBAN, IMRUDISHE TU IVO MAPUNDA

Picha
YALIKUWA maamuzi ya kukurupuka na yasiyokuwa ya kitaaluma kumtema kipa mahiri Ivo Philip Mapunda kwa kisingizio kisicho na maana yoyote, ilikuwa rahisi Simba kumpa mkataba kipa Vincent Angban raia wa Ivory Coast, pia ilikuwa ngumu kumpa mkataba mpya Ivo Mapunda. Bado kikosi cha Simba kinamuhitaji kipa kama Ivo Mapunda, Simba inaonekana ina mapungufu langoni kwake, mechi zote ilizocheza za ligi kuu bara, amedakaPeter Manyika Jr. Manyika Ndiye yule aliyepigiwa hesabu za kutolewa kwa mkopo, ndiye yule aliyepotezewa na mashabiki na baadhi ya viongozi kutokana na dharau zake alizozionyesha msimu uliopita, lakini Muingereza Dylan Kerr aliamua kumtumia katika mechi tano za mwanzo ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara na kuonyesha kiwango. KWANINI PETER MANYIKA JR Dylan Kerr aliamua kumtumia Peter Manyika Jr kwenye mechi zake za mwanzo mznguko wa kwanza ligi kuu bara baada ya kumuona katika michezo ya kirafiki iliyofanyika Zanzibar. Simba iliweka kambi yake Visiwani Zanzibar hivyo ...