FREEMASON YAMTESA MKOLA MAN, WAZAZI WAKE WAMJIA JUU.
Kuhusishwa kwa msanii wa hip hop wa mkoani Tanga Mkola Man na dini ya kishetani ya Freemason kumewashitua wazazi wake ambapo wamemjia juu na kutaka awathibitishie nini anachotaka kuwafanyia mpaka kuingia kwenye imani hiyo mbaya.
Wakizungumza na Mambo uwanjani, wazazi hao wamesema kuwa mtoto wao amejiunga kwenye dini hiyo ikiwa wao ni walokole, 'tunanyooshewa vidole na watu tunapokuwa kanisani na ikafikia hatua tukaanza kutengwa', walisema.
Lakini wakadai walipopata ukweli kuwa mtoto wao (Mkola Man) ni freemason wakamtaka aeleze ukweli iweje ajiunge na dini hiyo, akiwajibu wazazi wake, Mkola Man alisema yeye si freemason ila aliamua kujiita hivyo ili ajulikane.
Hata hivyo Mkola Man yupo katiak majuto baada ya kukimbiwa na jamaa zake wakihofia kutolewa kafara, Mkola Man anatamba na wimbo wake 'Jana na leo'