Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KOCHA TOTO AFRICANS AACHIA NGAZI, NI YULE MJERUMANI, NJAA YATAJWA

KOCHA Mjerumani wa Toto Africans ya Mwanza, Martin Grelis ameachia ngazi katika timu hiyo, akitoa sababu zaidi ya tatu, kubwa ni wachezaji kutothaminiwa na uongozi mbovu wa timu.
Grelis aliyeanza kazi Julai mwaka huu, amesema kwamba ameamua kuacha kazi baada ya kugundua hata wachezaji hawalipwi mishahara.

Aidha, safari za ‘kigumu’ kwenda mikoa ya Tanga na Tabora katika mechi zao za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara nazo zimechangia kumfanya aachie ngazi, ingawa mwenendo wa timu si mbaya hadi sasa.
“Kwa mwezi mzima tumefanya mazoezi ya uhakika mara saba tu, hali ambayo kocha yeyote hawezi kukubaliana nayo, nami kama kocha, imenilazimu kuchukua uamuzi huu ambao ungechukuliwa na kocha yeyote,”amesema.


Aidha, Grelis amesema kwamba wachezaji kutothaminiwa na kwa ujumla uongozi mbovu wa timu, navyo vimemfanya ashindwe kabisa kuendelea na kazi katika timu hiyo ya Mtaa wa Kishamapanda, Mwanza.

Hata hivyo, Grelis amesema anaamini kujiuzulu kwake kutaufanya uongozi ubadilike na kurekebisha mwenendo wake ndani ya timu, akiamini Toto ina wachezaji wazuri watakaoifanya timu iwe imara.
“Naamini, Toto ni timu yenye wachezaji wazuri, ambao wataifanya timu iweze kushindana na timu bora na kudumu katika Ligi Kuu. Itakuwa majanga sana iwapo, uongozi utashindwa kuwatimizia wachezaji mahitaji yao, ili waweze kucheza vizuri,”amesema.

Grelis anaiacha Toto ikiwa katika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuvuna pointi 10 katika mechi nane.

Mara ya mwisho, Grelis alikuwa kwenye benchi la Toto ikifungwa mabao 4-1 na Yanga SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na amesema matokeo hayio hayahusiani na kujiuzulu kwake.

Toto inatarajiwa kushuka tena dimbani kesho, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kumenyana na Mgambo Shooting ya Tanga katika mfululizo wa ligi hiyo.
Kwa ujumla, Ligi Kuu inaendelea kesho, mbali na Toto na Mgambo- pia Mwadui FC watakuwa wenyeji wa Yanga SC Uwanja wa Kambarage Shinyanga, Simba watakuwa wenyeji wa Coastal Union Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa ndugu zao Kagera Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.

Mechi nyingine, Mbeya City watakuwa wenyeji wa Majimaji FC Uwanja wa Sokoine, Ndanda FC wataikaribisha Stand United Uwanja wa Nangwanda, Mtwara wakati keshokutwa JKT Ruvu watamenyana na Azam FC Uwanja wa Karume, Dar es Salaam na Prisons wataikaribisha African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa