KIPA MPYA AIBEBA LIVERPOOL IKISHINDA KWA MBINDE KOMBE LA LIGI
KIPA mpya wa Liverpool, Adam Bogdan usiku wa jana alikuwa shujaa Uwanja wa Anfield baada ya kuokoa penalti tatu na kuiwezesha timu hiyo kutinga Raundi ya Kombe la Ligi England. Liverpool ilishinda kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 1-1 na Carlisle ya Ligi Daraja la Nne England katika michuano ya Capital One. Mchezaji mwingine mpya, Danny Ings alianza kuifungia Liverpool kipindi cha kwanza kabla ya Derek Asamoah kuisawazishia Carlisle na mchezo ukaenda kwenye dakika 30 za nyongeza. Penalti za Liverpool zilifungwa na Milner, Can na Ings wakati Lallana na Coutinho walikosa na za Carlisle zilifungwa na Dicker na Mcqueen huku Grainger, Joyce na Hery wakikosa. Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Bogdan, Clyne/Ibe dk86, Lovren, Milner, Firmino/Origi dk35, Moreno, Lallana, Can, Allen/Coutinho dk64, Ings na Skrtel. Carlisle: Gillespie, Miller, Raynes, Grainger, McQueen, Kennedy/Gillesphey dk73, Dicker, Joyce, Sweeney/Ibehre dk65, Hery na Asamoah/Gilliead dk64.