DK SLAA AZIDI KUIPASUA UKAWA, SASA NI JUMA NATURE NA MSAGASUMU WAREJEA CCM

Wanamuziki mahiri Juma Nature na Msagasumu ambao siku ya uzinduzi wa kampeni za kumnadi mgombea wa urais wa Chadema kupitia mwamvuli wa Ukawa Edward lLowasa zilizofanyika ktk viwanja vya jangwani wametangaza kuachana na Ukawa na kutangaza kurejea CCM.

Taarifa zilizotufikia hivi zinasema kuwa Nature na Msagasumu wameachana na ukawa na kurejea CCM baada ya kuchoshwa na siasa za majitaka zinazoendelea katika umoja huo wa katiba Ukawa, awali Nature alikuwa chama cha wananchi CUF na aliwahi kutangaza kugombea udiwani kupitia chama hicho lakini ikashindikana, na kuibukia kwenye kampeni za jangwani.


Pia inasemekana kilichowaondoa Ukawa ni kauli iliyotolewa na aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema Dk Willbroad Slaa hivi karibuni ambapo aliuponda umoja huo kwa uamuzi wao wa kumpokea Edward Lowassa ambaye alimtuhumu kwa kashfa ya ufisadi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA