MAKALA: TFF ISOGEZENI MBELE MECHI YA SIMBA NA YANGA KUPISHA KAMPENI ZA UCHAGZUI MKUU
Kampeni za kuwanadi wagombea wa nafasi za ubunge, udiwani zimepamba moto kila mahari, watu wako bize na siasa, kubwa zaidi ni nafasi ya mgombea wa urais, vyama mbalimbali vinajaribu bahati yao kwa kuzunguka nchi nzima kuwanadi wagombea wao.
Vyama vikuu CCM, Chadema kupitia mwamvuli wa Ukawa vinachuana vikali kuisaka dola, CCM yenyewe imeamua kumsimamisha mgombea wake wa urais Dk John Pombe Magufuli wakati Ukawa imemsimamisha mgombea wake Edward Ngoyai Lowassa.
Mchuano umekuwa mkali, kila mgombea anakubalika na watu wake hivyo kwa sasa habari inayozngumzwa kila sehemu ni uchaguzi mkuu, watu wameamua kuacha shughuri zao na kuwafuata wanasiasa wanaojinadi majukwaani wakiomba kura.
Siasa inatawala akili zetu kwa sasa, kuanzia kwenye daladala au vijiweni hata mahospitalini stori inayozungumzwa sana na kupewa nafasi kubwa ni siasa hasa uchaguzi mkuu, kila mmoja anasema lake, hata kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa Afrika AFCON zitakazofanyika Gabon kati ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Nigeria, Super Eagles uliofanyika jumamoso iliyopita siasa ilichukua nafasi yake.
Naibu waziri wa sayansi na teknolojia January Makamba ambaye pia ni mgombea ubunge wa jimbo la Bumbuli Tanga kupitia CCM aliamua kugharamia kiingilio ili mashabiki wa soka waliojazana nje ya uwanja wa Taifa kuingia ili kuipa nguv Stars.
Katika mchezo huo, Stars ilihitaji ushindi hivyo Makamba aliona ni vema akawalipia viingilio mashabiki hao ili kuipa sapoti timu yao na iweze kuibuka na ushindi, lakini mh Makamba badala ya kukaa kimya ili mashabiki hao waishangilie timu yao kumbe yeye alifanya hivyo ili kujipigia kampeni jimboni kwake.
Makamba alitumia nafasi hiyo kujinadi kwa kusema CCM oyeee, jukwaa wanalokaa mashabiki wa Simba walionyesha ishara ya vidole viwili inayotumiwa na Chadema kisha kuanza kuimba Lowassa...Lowassa...Lowassa, hali ile iliweza kuleta tafrani kwa dakika kadhaa kabla ya Makamba hajaondoka uwanjani kwa aibu.
Lakini mechi hiyo ilikuwa ya timu ya taifa, timu ambayo inaungwa mkono na Watanzania wote bila kujali Usimba wala Uyanga.
Kikosi cha Simba
Tanzania ina dini kubwa mbili tu ambazo ni Uilsamu na Ukristo yaliyobakia ni madhehebu tu na si dini, kila umuonaye ujue ni mmoja kati ya waumini wa dini hizo mbili, ingawa wapo pia wasiokuwa na dini ila siyo wengi sana.
Pia kuna timu kubwa zenye mashabiki wengi mbili tu ambazo ni Simba na Yanga, hizi ni klabu za soka, kati ya Watanzania milioni 48 wamejigawa makundi mawili na kuziunga mkono timu hizo, ni timu zenye mashabiki wengi kuliko timu zozote katika ukanda huu wa Afrika mashariki.
Ratiba iliyotolewa na Shirikisho la kandanda nchini TFF inaonyesha kwamba timu hizo kongwe na kubwa hapa nchini zitakutana Septemba 26 mwaka huu katika uwanja wa Taifa ukiwa ni mchezo wa raundi ya tatu ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, pia ni duru la kwanza la ligi hiyo ya msimu wa 2015/16.
Kwa nahati mbaya sana Simba na Yanga zinakutana wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, akili za Watanzania zipo kwenye siasa, ushabiki wa mpira wameweka kando, watu wanashabikia siasa.
Makada wa vyama vyote vya siasa ndio hao hao wapenzi na mashabiki wa Simba na Yanga, wagombea wa udiwani, ubunge na urais ndio hao hao wapenzi na mashabiki wa Simba na Yanga, na siku za kampeni huwa jioni kuanzia saa 8 hadi 12, wakati mechi ya Simba na Yanga nayo huchezwa jioni kuanzia saa 8 mageti yanafunguliwa na huanza saa 10 hado 12.
Mashabiki wengi wa soka watakaojitokeza uwanja wa Taifa ndio hao hao wanaotakiwa kuudhuria mikutano ya kampeni, hivyo ningeliomba Shirikisho la kandanda nchini TFF kuangalia umuhimu wa uchaguzi huo mkuu na ukubwa wa mechi ya Simba na Yanga.
Kwani kuna umuhimu gani mechi hiyo kuchezwa mwezi huu wa kampeni za uchagzui mkuu, kwanini mechi hiyo isipelekwe hadi Novemba, TFF inapaswa kuwaachia Watanzania kushiriki vema kampeni na uchaguzi mkuu wa nchi.
Mechi ya Simba na Yanga nchi inasimama, hivyo ni vema Watanzania wakaachwa kufanya harakati zao za kisiasa, ninaamini Simba ina wanachama wake pamoja na mashabiki ambao wapo pia CCM, Ukawa na vyama vinginevyo.
Vile vile mechi ya Simba na Yanga inaweza kutumika kisiasa, kama ilivyokuwa kwa mchezo wa timu ya taifa, Taifa Stars ilipocheza na Nigeria, Super Eagles, yasije kutokea yale yalitokea Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Taifa.
Kikosi cha Yanga
Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa mkali na wa aina yake hivyo kila chama kitatumia fulsa hiyo kujitangaza, kwakuwa vyama vyote vyote viwili vyenye ushindani mkubwa vimesimamisha wagombea wake wanaokubalika na wananchi, kuna wasiwasi vyama hivyo vikazitumia klabu hizo kama daraja la kuingia Magogoni maarufu Ikulu.
Ni vema TFF kwa kushirikiana na Bodi la ligi wakasikiliza kilio changu na cha Watanzania kwa ujumla na kuamua kuisogeza mbele mechi hiyo, tayari nina hofu na wanamichezo kuguswa na siasa za sasa na kutaka kuchanganya mambo ya soka na siasa hivyo ni bora soka libakia kuwa soka na siasa ibakie kama siasa kila mmoja achukue mkondo wake.
Wapo wanamichezo wasiopenda kushabikia siasa lakini pia wapo wanamichezo wanaopenda kuingilia siasa, ni vema kila kimojawapo kifanyike kwa wakati wake, wanamichezo ni kioo cha jamii hivyo kushabikia siasa ni hatari kwani kunaweza kuleta mgawanyiko mkubwa, hii inatokea pale anapoanguka unayemuunga mkono ambapo kunauwezekano aliyeshinda asikupe ushirikiano wa kutosha na zikaanza lawama kwamba mnaonewa