Drogba naye awafuata akina Henry, Gerrald Marekani
Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba amekamilisha usajili wake kwenye klabu ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS), Montreal Impact ya Canada. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 ambaye alikuwa nahodha wa Ivory Coast ametua Montreal kama mchezaji huru baada ya kumaliza maisha yake katika klabu ya Chelsea alikorejea akitokea China alikocheza kwa msimu mmoja. Aliichezea Chelsea kwa mafanikio na kufunga mabao 164 kwa misimu tisa. Awali, Drogba alivumishwa kuwa angetua Inter Milan na klabu nyingine la MLS ,Chicago Fire ambayo zilikuwa zikimtaka. Hata hivyo, Drogba aliichagua Montreal Impact ambayo amesaini mkataba wa kuichezea msimu ujao.