KIMONDO YAZIDI KUIWEKA ROHO JUU YANGA
Wakati uongozi wa Yanga umedai kuwa ulimsajili kiungo Geofrey Mwashiuya akiwa huru, uongozi wa Kimondo umesema una mkataba na mchezaji huyo na utawashtaki mabingwa hao wa Bara ikiwa wataendelea kumtumia.
Mwanzoni mwa wiki Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18, alisaini nayo mkataba wa miaka mitatu akiwa huru.
Hata hivyo, mkurugenzi wa Kimondo, Elick Ambakisye aliuambia mkutano na waandishi wa habari jijini hapa jana kuwa Mwashiuya ana mkataba wa miaka minne aliousaini Agosti 30 mwaka jana.
"Mchezaji (Mwashiuya) mwenyewe alisaini mkataba huu (anauonyesha). Endapo Yanga wataendelea kumng'ang'ania na kumtumia mchezaji wetu, tunajua wanashiriki Kombe la Kagame mwezi huu, tutawashtaki katika mamlaka husika," alisema Ambakisye.
Kombe la Kagame la klabu bingwa ya Afrika Mashariki na Kati linashirikisha wachezaji waliosajili na kupata leseni za kuzitumikia klabu.
Hivyo ni wazi kwamba Yanga haitamtumia Mwashiuya kwa sababu usajili wake bado haujaidhinishwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka (TFF).
Mwashiuya alijiunga na Yanga mwezi uliopita na kuibua mvutano kati ya viongozi wa timu yake hiyo mpya na Kimondo.
Kiungo huyo anayetumia mguu wa kushoto alionyesha kiwango kizuri katika mechi yake ya kwanza ya kiamataifa ya kirafiki ambayo Yanga ilitoka suluhu na SC Villa ya Uganda, kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi iliyopita.
Mbali na Mwashiuya, Yanga imesajiliwa pia wachezaji wazawa wengine Deus Kaseke kutoka Mbeya City, Malimi Busungu (Mgambo JKT), Benedicto Tinocco (Kagera Sugar) na Haji Mwinyi Mgwali (KMKM).
Pia imewachukua Mzimbawe Donald Ngoma na Mghana Josephat 'Teteh' Zhuta.
Mbali na Kombe la Kagame ambako Yanga itakuwa ikiwania kufikia rekodi ya watani wa jadi ya kuchukua ubingwa mara ya sita, timu hiyo inajiandaa kutetea taji la ligi kuu ya Bara na kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Afrika mwakani.