KOCHA SIMBA AZIOGOPA YANGA, AZAM
Kocha wa Simba, Dylan Kerr amesema anahitaji mechi tano za kirafiki kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Bara, lakini si dhidi ya Yanga na Azam.
Kocha huyo Mwingereza alianza kibarua chake juzi aliliambia gazeti hili kuwa anahitaji mechi hizo za kirafiki dhidi ya timu yoyote inayoshiriki Ligi Kuu, lakini isiwe Azam wala Yanga kwani anajua hao ni wapinzani wake katika mbio za kusaka ubingwa.
Simba iliyoanza mazoezi ya viungo gym wiki iliyopita, juzi ilianza mazoezi ya uwanjani chini ya kocha Kerr na wasaidizi wake, Selemani Matola, Mserbia Dusan Momcilovic kocha wa viungo na kocha wa kipa, Mkenya Abdul Iddi Salim.
“Nahitaji mechi za kirafiki kama tano ili kuwajua vizuri wachezaji wangu na kujua upungufu wa kikosi changu kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.
“Tutacheza na timu yoyote ya Ligi Kuu ikiwa tutafanikiwa kupata timu za kucheza nayo, lakini isiwe Yanga au Azam ambazo najua ni wapinzani wetu, hata kwenye mbio za ubingwa,”alisema.
Pia, Mwingereza huyo ameanza kazi kwa kuwapiga mkwara wachezaji wavivu wa timu hiyo na kuwaambia kuwa hatakuwa na urafiki nao anayejijua ni mvivu hafai katika kikosi chake.
“Napenda wachezaji wanaojituma na sitakuwa rafiki wa mchezaji mvivu, mchezaji wa namna hiyo atapata shida kwangu,” alisema.
Pia, Kerr alisema kikosi chake kinatarajia kuweka kambi ya muda mrefu Lushoto mkoani Tanga kuanzia Jumatatu kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi.
Kocha huyo asiye na masihara uwanjani alisema baada ya kambi hiyo ya Lushoto watakwenda Zanzibar kuweka kambi ya muda tayari kwa Ligi Kuu Bara inayoanza Agosti.
“Tunatarajia kwenda Lushoto kuweka kambi huko, ni sehemu ya baridi, nimefanya hivyo kwa sababu timu inahitaji kufanya mazoezi magumu na kama unafanya mazoezi ya aina hiyo kukaa sehemu hiyo ni nzuri,” alisema kocha huyo.
Kerr amejiunga na Simba hivi karibuni akichukua mikoba ya Mserbia Goran Kopunovic aliyeinoa Simba msimu uliopita, lakini alishindana dau na uongozi wa klabu hiyo na kuamua kuondoka.