Simba yaendeleza mauaji Zanzibar, yaipiga Black Sailor 4-0

Simba imetoa mafunzo ya soka kwa tiku ya Black Sailor  kwa kuichapa kwa mabao 4-0.Black Sailor ambayo imepanda Ligi Kuu Zanzibar msimu huu ilikiona cha moto, kwani hadi mapumziko Simba ilikuwa ba mabao mawili.

Abdi Banda ndiye alianza kuifungia timu yake bao dakika ya nne tu baada ya kupokea pasi nzuri ya Dani Alves au Hassan Kessy na Kadabra Ibrahim Ajib akaongeza la pili katika dakika ya 23.

Simba ilipata mabao yake mengine katika dakika dakika 80 na 90 wafungaji wakiwa ni Elius Maguli na Boniface Maganga.


Wakati wote, Kocha Dylan Kerr alikuwa akisisitiza timu hiyo kucheza kwa kushambulia sana.

Hii ni mechi ya pili ya kirafiki ya Simba mjini hapa, mechi ya kwanza ilishinda kwa mabao 2-0, yaliyofungwa na mkongwe Mgosi na Hamis Kiiza.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA