Drogba naye awafuata akina Henry, Gerrald Marekani

Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba amekamilisha usajili wake kwenye klabu ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS), Montreal Impact ya Canada.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 ambaye alikuwa nahodha wa Ivory Coast ametua Montreal kama mchezaji huru baada ya kumaliza maisha yake katika klabu ya Chelsea alikorejea akitokea China alikocheza kwa msimu mmoja. Aliichezea Chelsea kwa mafanikio na kufunga mabao 164 kwa misimu tisa.

Awali, Drogba alivumishwa kuwa angetua Inter Milan na klabu nyingine la MLS ,Chicago Fire ambayo zilikuwa zikimtaka.

Hata hivyo, Drogba aliichagua Montreal Impact ambayo amesaini mkataba wa kuichezea msimu ujao.


Chicago Fire, ilikuwa ikisaka saini yake kwa miezi tangu amalize mkataba wake wa kuichezea Chelsea ilikaribia kumnasa, lakini akaponyoka dakika za mwisho.

Dogba ameichagua Montreal, ambayo ni sehemu ya Canada, ambayo wakazi wake wanazungumza Kifaransa, lugha ambayo anaielewa vizuri, ambako atakuwa akilipwa Dola 250,000 kwa wiki kulingana na vyanzo mbalimbali.

Rais wa Montreal Impact, Joey Saputo aliuambia mtandao wa klabu hiyo: “Ni heshima kwa kila mmoja wetu kumpata mtu kama Didier Drogba kwenye klabu yetu.

“Kutokana na mazungumzo baina yetu, ninaamini amefurahia maisha hapa Montreal ambako atacheza soka na kuishi. Ni siku muhimu katika historia ya klabu yetu, atakuwa faida kwa kila hali.”

Bosi wa Chicago Fire, Frank Yallop alieleza: “Ningependa kuwa na Drogba, lakini amechangua Montreal, hakuna kitu tunachoweza kufanya. Montreal ni eneo ambako wanazungumza Kifaransa, yeye na familia yake wataishi vizuri.”

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA