MAKALA: SHUKURU NASSORO 'SHAMTA' MSANII ANAYEICHIPUKIA, ADAI YOUNG D NDIYE ALIYEMFANYA AIMBE HIP HOP
Na Mwandishi Wetu
ANAFAHAMIKA zaidi kama Shukuru Nassoro jina ambalo alipewa na wazazi wake wawili baba na mama, lakini vijana wenzake wa mtaani wakampachika jina la utani Shamta ambalo ndilo analolitumia kwenye sanaa yake ya muziki wa hip hop.
Shamta alizaliwa Machi 27 mwaka 1996 Mdaula Chalinze mkoani Pwani, na ni mtoto wa sita kuzaliwa katika familia ya mzee Nassoro, elimu yake ya msingi aliianzia hapo hapo Mdaula na mwaka 2012 akabahatika kufaulu na kujiunga na sekondari.
Msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya alichaguliwa kujiunga na sekondari ya Handeni mkoani Tanga ambapo mwaka huu anatarajia kumaliza kidato cha nne na kujikita kisawa sawa kwenye muziki.
Akielezea muziki, Shamta anasema alianza kuupenda muziki tangia anasoma shule ya mdingi na alizidi kuupenda kila alivyozidi kukua, Shamta anadai Young D ndiye aliyemsukuma zaidi kuingia kwenye tasnia hiyo inayopendwa na vijana wengi hapa nchini, hivyo naye aliamua kuingia rasmi kwenye gemu.
Anaongeza kuwa alijifunza mengi kupitia kwa msanii huyo na ndipo na yeye alipoanza kuimba kwa freestyle ambapo watu mbalimbali wakaanza kumshangaa.
'Nilikuwa naimba style zote ili kuuzoea muziki wa hip hop na ujuzi wa kuimba freestyle ambapo watu wakapagawa kwa kipaji changu', alisema Shamta.
Kwa sasa tayari amesharekodi nyimbo tatu ambazo ni 'Maisha yangu', 'Mgombea Tanzania' na Bodo In Fany.
Na hivi karibuni alikuwa akimalizia kutengeneza video ya wimbo wake wa 'Mgombea Tanzania' unaoelezea uchaguzi mkuu, Shamta ameamua kutengeneza wimbo maalum unaohusu uchaguzi ambapo wagombea mbalimbali hujitokeza mbele za wanachi na kujinadi kwa maneno mazuri, lakini wakishapata uongozi hawaonekani tena.
Hata hivyo msanii huyo amemsifu prodyuza chipukizi Side Kichwa ambapo amekuwa akimtengenezea beat kali pamoja na mixer sound za nguvu licha ya kufanya kazi na prodyuza huyo, Shamta amedai anaweza kuafanya kazi na prudyuza mwingine ila Side Kichwa ataendelea kumuheshimu.
Hakusita kutoa shukrani zake kwa Shaaban Hussein 'Presha wa Mdaula' ambaye amekuwa akimsaidia kwa mambo mbalimbali ikiwemo kumtafutia wadhamini, pia amelipongeza gazeti hili kwa kuwajali wasanii chipukizi kama yeye.
Mwisho, msanii huyo amedai anategemea kuutangaza muziki wake kimataifa, amedai muziki unalipa endapo tu atafanikiwa kukubalika na mashabiki, Shamta anasema anataka kuyafikia japo mafanikio ya msanii Young D