Machapisho

Barker kocha pekee aliyeshinda mechi 9 Ligi Kuu bara

Picha
Na Nasri Khalfan  Steve Barker kocha pekee aliyeshinda michezo yake yote tisa ya Ligi Kuu msimu huu, hakuna sare wala kupoteza. Amekusanya alama 27 kati ya 27 zinazowezekana, maximum points na kuifanya Simba kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi kwa tofauti ya alama tano dhidi ya wapinzani wao, Young Africans. Kocha pekee kwenye Ligi yetu ambaye hajawahi kuonja ladha ya kipigo msimu huu

Yanga kumrudisha Ramovic

Picha
Inasemekana viongozi wa klabu ya Yanga SC wanakaribia kumrekesha aliyekuwa kocha wake Mjerumani Seaf Ramovic badala ya kushindikana kumchukua kocha wa zamani wa Pyramid ya Misri. Taarifa zenye uhakika zinasema kwamba Ramovic anawasili nchini na Jumapili atakuwrpo uwanjani kuishuhudia Yanga ikiumana na Kagera Sugar.

Simba yapata ushindi kiduchu

Picha
Timu ya Simba jioni ya leo imechomoza na ushindi kiduchu wa goli 1-0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara. Fountain Gate inayonolewa na beki wa zamani wa Yanga Fred Felix Minziro, walikuwa na mchezo mzuri kiasi kwamba walitaka kuibana Simba na kulazimisha sare. Bao pekee la Simba lilifungwa na beki wake wa kati Rushine De Reuck dakika ya 35, kwa ushindi huo sasa Simba insfikisha pointi 27 ikiwa imecheza mechi 9 na Iko kileleni kwa tofauti ya alama 5 na hasimu wake Yanga anayeshika nafasi ya pili.

Uchaguzi Simba umeiva

Picha
“Tarehe 30 Oktoba, 2026 hadi tarehe 6 Novemba, 2026 litakuwa ni zoezi la kuchukua fomu kwa wagombea, tarehe 7-11 Novemba, 2026 itakuwa ni zoezi la kurudisha fomu kwa wale ambao wamechukua. Tarehe 12-14 Novemba, 2026 litakuwa zoezi la kupitia zile fomu, kuzikagua, kuzihakiki kama zimejazwa inavyotakiwa na kutangaza majina ya waliokidhi vigezo vya kugombea. Tarehe 15 Novemba, 2026 itakuwa ni siku ya kutangaza majina ya wagombea waliokidhi vigezo na kukaribisha mapingamizi dhidi ya wagombea, tarehe 17-18 Novemba, 2026 kitakuwa kipindi cha kupokea mapingamizi, tarehe 19-21 Novemba, 2026 itakuwa ni kupitia yale mapingamizi pamoja na kuandaa hati za wito kwa waliowasilisha mapingamizi pamoja na waliowekewa mapingamizi, tarehe 23-25 Novemba, 2026 itakuwa ni kipindi cha kusikiliza mapingamizi, tarehe 26-27 Novemba, 2027 itakuwa ni kutoa mapingamizi dhidi ya wagombea, tarehe 30 Novemba, 2026 itakuwa ni siku ya kutangaza majina ya waliofuzu au majina ya waliokidhi vigezo vya kugombea.” “Tarehe 3...

Azam FC yaifukuzia Yanga Ligi Kuu bara

Picha
Wauza lambalamba wa Azam FC usiku huu imeichakaza bila huruma timu ya Mbeya City ya mkoani Mbeya mabao 4-0 mchezo wa Ligi Kuu bara uwanjani wa Azam Complex Chamazi Dar es Salaam. Mabao pekee ya Azam FC yamefungwa na Iddi Seleman Nado dakika ya 45, Feisal Salum Feitoto' dakika ya 62, Hassan Mubiru dakika ya 71 na Kipre Emmanuel Jr dakika ya 89, ushindi huo unaifanya timu hiyo kufikisha pointi 20 wakiwa na michezo 9 wakishika nafasi ya tatu.

Aziz Ki amenifukuzisha Yanga- Manqoba

Picha
“ Nikiwa Mkweli tatizo halikuwa Kuhusu Kumchezesha Stephanie Aziz Ki Kwasababu Viongozi walikuwa na uhakika akirejea Kwenye fitness yake atasaidia timu“ “ Lakini tatizo ni Kwamba kuna Uwezekano Aziz Ki amezungumza na baadhi ya Viongozi Kwamba hafurahishwi na Mfumo wangu “ “Kwasababu Kwenye mfumo wangu yeye ndo anatakiwa Kuweka Presha wa Kwanza wakati wa Kukaba. Anatakiwa kuhusika na Mchezo Kwenye phases zote” “Lakini Kusema tulikuwa na tatizo binafsi nitakuwa nadanganya”.Tatizo ni atakuwa na uwezo Kukimbia Kwenye team Yangu?” “Kwenye team Yangu namba 10 anatakiwa kuhusika Kwenye Kila tukio wakati timu yangu Inashambulia” “Hatuwezi Kuwa na namba 10 ambaye anagusa Mpira Kila baada ya Dakika 10 au 15” Source Metro FM na Soccer Laduna.

Barker aingia mchecheto na Berkane na Orlando

Picha
Kocha wa Simba SC, Steve Barker, amekiri kuwa Kundi lao la Ligi ya Mabingwa Afrika ni gumu, akizitaja RS Berkane ya Morocco na Orlando Pirates ya Afrika Kusini kuwa wapinzani wenye ushindani mkubwa. Barker amesema anaifahamu vizuri RS Berkane kutokana na kukutana nayo akiwa na timu zake za zamani, huku Orlando Pirates akiwa ameizoea kutokana na uzoefu wake wa soka la Afrika Kusini. Kuhusu Colombe Sportive ya Cameroon, amesema licha ya kuwa ni mara yao ya kwanza kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba hawapaswi kuwadharau. “Ukitaka kufika mbali katika mashindano haya, lazima uvuke hatua ya makundi bila kujali wapinzani unaokutana nao,” amesema Barker, akisisitiza kuwa lengo lao ni kuhakikisha Simba inafuzu hatua ya mtoano. soba_minerals_investment