Machapisho

Simba yaendeleza umwamba Misri

Picha
TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wadi Degla SC inayoshiriki Ligi Daraja la Pili A Misri katika mchezo wa kirafiki leo Jijini Cairo. Mabao ya Simba SC katika mchezo wa leo yamefungwa na viungo washambuliaji, Kibu Denis Prosper na Mkongo, Elie Mpanzu Kibisawala huo ukiwa mchezo wa nne katika kambi ya timu hiyo kujiandaa na msimu mpya nchini Misri. Katika mechi tatu za awali kwenye kambi yake ya kujiandaa na msimu nchini Misri — Simba ilishinda mbili na kufungwa moja. Ilishinda 1-0 Jijini Cairo dhidi ya Al Zulfi inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Saudi Arabia na 2-0 Jijini Ismailia dhidi ya Carabat FC inayoshiriki Ligi ya Kanda nchini Misri, wakati mechi nyingine ilifungwa  4-3 na ENPPI ya Ligi Kuu ya Misri Jijini Cairo. Simba SC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids raia wa Afrika Kusini kesho inatarajiwa kucheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Liberia, FC Fassell. Baada ya hapo Simba SC itarejea nchini tayari kwa tamasha la...

Madagascar yatinga fainali mataifa Afrika CHAN

Picha
TIMU ya Madagascar imefanikiwa kutinga Fainali ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Bao pekee la Madagascar katika mchezo huo uliodumu kwa dakika 120 baada ya dakika 90 kumalizika timu hizo zikiwa hazijafungana limefungwa na winga wa Saint-Denis FC, Toky Niaina Rakotondraibe dakika ya 116. Madagascar sasa itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kati ya mabingwa watetezi, Senegal na Morocco zinazomenyana usiku huu Uwanja wa Mandela Jijini Kampala, Uganda. Fainali ya CHAN 2024 itapigwa Agosti 30 Uwanja wa Moi International Sports Centre, Nairobi nchini Kenya ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Agosti 29 Uwanja wa Mandela, Kampala.

Mchambuzi Wasafi akandia Simba kuwaaga Bocco na Mkude

Picha
Ningekuwa Mkude au John Bocco nisingependa siku ya tukio la kuagwa na Simba kwa sababu Simba wana mtindo wa kuchafua taswira za Malegend wao kwa makusudi kabisa Ameondoka Aishi Manula hawajampa heshima yoyote kabisa na hajaenda Yanga ameenda Azam  kwanini sahivi Aishi hapewi Ile thamani ya Legend ndani ya Simba nani alie ichafua hiyo thamani ni Simba wenyewe  Simba Wana wachezaji wengi walio ipambania Ile klabu kwa jasho lao lote wakati wa mafanikio walivyokuja kuondoka heshima yao yote imefutwa sasa hivi ukimtaja Aish ndani ya Simba ni kama hamna kitu kwa jinsi walivyoichafua taswira yake  Angalia Mazingira ya Mohamed Hussein kuondoka kosa lake ni nini? Mohamed Hussein ameshindwana na Simba kimaslahi amepata sehemu yenye maslahi bora zaidi kama mchezaji angefanya nini  Mfano Yanga wameachana na Khalid Aucho misimu huu baada ya kushindwana kwenye masuala ya kimkataba umesikia sehemu yoyote Yanga wakichafua taswira ya Aucho". Mchambuzi Nasri Khalfan akizungumza kupiti...

CS Constantine yaitumia ofa Simba kwa Kibu

Picha
Klabu ya CS Constantine kutoka Algeria Imewasilisha Rasmi Ofa ya Kumsajili Kibu Deniss Kutoka Simba. Klabu  hiyo ya Algeria iliweka mezani ofa yenye thamani ya dola 180,000, chini kabisa ya thamani ambayo Simba wanahitaji. Kwa Mujibu wa Taarifa kutoka Simba ni kuwa Simba wao wanahitaji  dola 350,000 ili kumuachia Kibu Deniss.

Simba yasogeza mbele uzinduzi wa jezi mpya

Picha
Klabu ya Simba Sc imetangaza kusogeza mbele tukio la uzinduzi wa jezi za klabu hiyo kutoka Agosti 27, 2025 kama ilivyopangwa awali na sasa hafla hiyo ya uzinduzi itafanyika Agosti 31, 2025, sababu ya mabadiliko hayo haijatajwa. Awali Wekundu hao wa Msimbazi walitangaza kuwa uzinduzi wa jezi hizo kwa ajili ya msimu mpya wa 2025/26 itafanyika Agosti 27, 2025 katika ukumbi wa SuperDome, Masaki kuanzia saa 1 usiku huku ikitaja kiingilio cha Tsh. 250,000 kwa shabiki anayetaka kuhudhuria uzinduzi huo.

Simba pasua kichwa kwa Okello

Picha
Klabu ya Simba SC haijatuma ofa rasmi kwenda Vipers SC ili kupata saini ya kiungo mshambuliaji Allan Okello (25) kuelekea msimu ujao Hakuna userious sana kwa Simba SC bali wanaonesha kuvutiwa nao na klabu kutoka Ubelgiji na Afrika Kaskazini zinahitaji saini yake

Baraka Majogoro ajiunga na KMC kutoka Afrika Kusini

Picha
Klabu ya KMC FC imekamilisha usajili wa kiungo Baraka Majogoro (27) kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi Majogoro amejiunga na KMC FC akitokea Chippa United ya Afrika Kusini ambayo ameachana nayo kuelekea msimu mpya