Machapisho

HABARI/PICHA:

Picha
WAKALI WA SOKA WALIPOKUTANA. Pichani, ni wachezaji waliopata kung' ara katika miaka ya hivi karibuni, (Kutoka kushoto ni mshambuliaji wa zamani wa Singida United ya mkoani Singida na Yanga SC ya Dar es Salaam, Kipanya Malapa mtoto wa Buguruni Malapa, katikati ni beki mahiri wa zamani wa Pamba FC ya jijini Mwanza, James Washokera wakiwa sambamba na Super Stoper, Khalid Ngome "Bitebo" mkali wa zamani wa Singida United, ambaye pia aliwahi kupita Simba SC, Yanga SC na klabu nyinginezo

WANACHAMA SIMBA KUMPA TIMU "MO" LEO

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Wanachama wa klabu ya Simba leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Ocean Road jijini Dar es Salaam wanakutana kupitisha mpango wa kumkabidhi klabu mfanyabiashara Mohamed 'MO' Dewji aliyekubali kumwaga shilingi Bilioni 20 kununua asilimia 49 za Hisa. Jana Simba ilikabidhiwa ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo iliumana na Kagera Sugar na kuchapwa bao 1-0. Kuelekea mkutano huo unaotazamiwa kuanza saa 3:00 asubuhi ulioitishwa na kaimu mwenyekiti Salim Abdallah "Try Again" Simba inaenda kufanya mabadiliko ya katiba ambayo sasa yanampa mwekezaji mpya asilimia 49 badala ya 51 kama walivyokubaliana mwanzo. Serikali kupitia wizara ya Michezo, Habari, Sanaa na Utamaduni ilizuia klabu kumuuzia Hisa 51 mtu mmoja na imetaka wanachama wasaliwe na asilimia 51 na mtu mmoja ahuziwe asilimia 49 jambo ambalo linaenda kutimia...

YANGA KAMA POMBE YA NGOMANI, KILA MTU ANAJICHOTEA, YACHAPWA 1-0 NA MWADUI

Picha
Na Paskal Beatus. Shinyanga Yanga SC imekuwa kama pombe ya ngomani ambapo kila mmoja hujichotea na leo jioni imedhihirisha hayo baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 toka kwa vijana wa Mwadui FC uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga. Huo ni mchezo wa tisa Yanga inacheza bila kupata ushindi na ikumbukwe mara yake ya mwisho kushinda ilikuwa dhidi ya Welayta Dicha mchezo ukiwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika ushindi wa mabao 2-0, na tangu aondoke kocha wake mkuu Mzambia George Lwandamina Yanga haijaonja ushindi zaidi ya kupata sare tatu ikifungwa mechi sita. Bao lililoizamisha Yanga, lilifungwa na kiungo chipukizi Awesu Awesu Ally kunako dakika ya 19, Yanga sasa tayari imeshajiondoa katika nafasi ya tatu kwani Azam FC kesho inaweza kushinda na kukaa mazima kwenye nafasi hiyo. Mechi nyingine leo timu ya Singida United imewachapa Majimaji Fc ya Songea mabao 3-1 yaliyofungwa na Deus Kaseke, Shafik Batambuze na Tafadzwa Kutinyu wakati la Majimaji likiwekwa kimiani na Jerry Tegete, m...

KAGERA SUGAR YATIBUA SHEREHE ZA UBINGWA SIMBA MBELE YA RAIS MAGUFULI, KASEJA AWA SHUJAA

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Timu ya Kagera Sugar ya Misenyi mkoani wilayani Bukoba mkoani Kagera jioni hii imefanikiwa kuilaza Simba SC na kutibua kabisa rekodi za klabu hiyo ya kutokufungwa hata mchezo mmoja pia kuharibu pilau lao leo mbele ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli ambaye leo alikuwa mgeni wa heshima. Simba wamekabidhiwa kombe lao la ubingwa wa Bara baada ya kulitwaa Mei 10 mwaka wakati wapinzani wao Yanga SC kuchapwa mabao 2-0 na Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Katika mchezo wa leo, Kagera Sugar walionekana kulinda zaidi lango vipindi vyote viwili, bao pekee la ushindi lilipatikana kipindi cha pili dakika ya 87 kupitia kwa Japhet Makalai, Simba walizawadiwa penalti lakini shuti la Emmanuel Okwi liliokolewa na kipa mkongwe Juma Kaseja. Baada ya mchezo huo kumalizika, Rais Magufuli alihutubia machache ambapo kikubwa alisema yeye ni shabiki wa timu ya taifa, Taifa Stars Kagera Sugar imeichapa Simba bao 1-0 leo

YANGA NA MWADUI VITANI LEO

Picha
Na Paskal Beatus. Shinyanga Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea tena leo kwa mechi nne kupigwa katika viwanja tofauti hapa nchini, saa nane ya mchana mtanange unaendelea katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kati ya Simba SC na Kagera Sugar ambapo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ni mgeni wa heshima. Lakini kazi itakuwepo mjini Shinyanga katika uwanja wa CCM Kambarage wakati wenyeji Mwadui FC inapowakaribisha Yanga SC saa 10, mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali kutokana na Yanga kuitamani nafasi ya pili ambayo kwa sasa inashikiliwa na Azam FC. Mchezo mwingine utakuwa kati ya Lipuli na Mbeya City, ligi hiyo itaendelea tena kesho jioni wakati Njombe Mji inawaalika Mtibwa Sugar ya Turiani na Azam FC itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons uwanja wa Azam Complex, Chamazi Yanga inaumana na Mwadui leo

MESSI APAGAWISHA MASHABIKI AFRIKA KUSINI

Picha
Uwepo wa mwanasoka Lionel Messi nchini Afrika Kusini kumezua hisia kubwa miongoni mwa mashabiki wa soka kwa siku tatu mfululizo baada ya mchezaji huyo nyota kutoka Argentina kufanya ziara nchini humo akiwa na timu yake ya Barcelona. Mshindi huyo wa mara tano wa tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa dunia, alishiriki katika mechi ya kirafiki kati ya timu yake ya Barcelona na Mamelod Sundows na kusaidia ushindi wa mabao 3-1. Kundi la wanamichezo hao wa Barcelona lililopata nyota lilifika Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki Jumatano iliyopita dhidi ya mabingwa wa Rainbow, Mamelod Sundows. Mchezo huo umekumbushia mchezo wao wa mwaka 2007, ulipigwa katika uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg ukiwa kama wa kuadhimisha miaka 100 ya Nelson Mandela Rais wa kwanza mweusi wa taifa hilo. Mandela aliwakilisha mapambano ya uhuru na usawa na alifanya jukumu kubwa katika kuunganisha jamii iliyogawanyika katika misingi ya ukabila, hiyo ni aina ya roho ambayo Barcelona daima inatambua...

SIMBA KUSAKA HESHIMA KWA MAGU, KAGERA KUTIBUA SHEREHE

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Macho ya Watanzania leo yanaelekezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati mabingwa wa Tanzania Bara Simba Sc watakapoumana na Kagera Sugar mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaoudhuriwa na Rais wa Jamhurri ya muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli. Rais Magufuli anakuwa mgeni wa heshima ambapo atakabidhi kombe la ubingwa wa Tanzania Bara kwa Simba Sc na pia ataikabidhi ubingwa wa Cecafa, timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys iliyoutwaa huko Kenya mwezi uliopita. Simba Sc imetawazwa kuwa mabingwa wa Tanzania Alhamisi ya Mei 10 mwaka huu baada ya wapinzani wao kwenye mbio hizo Yanga Sc kufungwa mabao 2-0 na Prisons. Hivyo katika mchezo wa leo Simba wanahitaji kushinda ili kulinda heshima yake na vilevile kutaka kuweka rekodi nyingine ya kumaliza ligi bila kufungwa, lakini Kagera Sugar yenyewe itataka kutibua sherehe za Wanasimba ambao wanafurahia ubingwa wao wa msimu huu walioutwaa kwa mara ya kwanza baa...