MESSI APAGAWISHA MASHABIKI AFRIKA KUSINI
Uwepo wa mwanasoka Lionel Messi nchini Afrika Kusini kumezua hisia kubwa miongoni mwa mashabiki wa soka kwa siku tatu mfululizo baada ya mchezaji huyo nyota kutoka Argentina kufanya ziara nchini humo akiwa na timu yake ya Barcelona.
Mshindi huyo wa mara tano wa tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa dunia, alishiriki katika mechi ya kirafiki kati ya timu yake ya Barcelona na Mamelod Sundows na kusaidia ushindi wa mabao 3-1.
Kundi la wanamichezo hao wa Barcelona lililopata nyota lilifika Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki Jumatano iliyopita dhidi ya mabingwa wa Rainbow, Mamelod Sundows.
Mchezo huo umekumbushia mchezo wao wa mwaka 2007, ulipigwa katika uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg ukiwa kama wa kuadhimisha miaka 100 ya Nelson Mandela Rais wa kwanza mweusi wa taifa hilo.
Mandela aliwakilisha mapambano ya uhuru na usawa na alifanya jukumu kubwa katika kuunganisha jamii iliyogawanyika katika misingi ya ukabila, hiyo ni aina ya roho ambayo Barcelona daima inatambua.
Messi hata hivyo alipata homa ya mafua na dakika ishirini kabla ya mpira kwisha aliingia uwanjani, alisababisha mashabiki kuweweseka kwa furaha na kupayuka kwa sauti pindi walipomwona nyota huyo akipasha